Saturday 6 February 2016

On 03:16 by Unknown   No comments

·        Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa
·        Afisa Maendeleo wa Mtaa
·        Mwenyekiti wa Kamati ya Afya na Mazingira
·        Wajumbe wa Serikali ya Mtaa
·        Mwenyekiti wa Maruhania
·        Katibu wa Maruhania
·        Waganga Mafundi, Walimu wa Maruhania (Watabibu wa Tiba Asilia)
·        Mabibi na Mabwana.
Habari za Muda huu
Leo ni siku ya pekee kwa wanamaruhania na watu wote wanaopenda maendeleo yetu na hasa katika tiba asilia na afya ya watanzania. Ni siku ambayo tunaandika historia katika Tiba Asilia na Maruhania. Kihistoria hakuna anayefahamu kwa hakika lini ushirikiano kati ya mwanadamu na Maruhani katika kutoa huduma ya Tiba Asilia na ilianza lini kutumika hapa kwetu Tanzania ila kila mmoja wetu atakubariana kuwa ilianza tuu pale binadamu wa kwanza alipoanza kuishi katika nchi yetu kwa miaka yote ya kuwepo kwa binadamu hapa Tanzania, Tiba ya kiruhani nayo imekuwa muhimili wa matibabu ya Tiba Asili.
Pamoja na kuwepo kwa maendeleo makubwa katika teknolojia na usambazaji wa huduma ya Tiba ya kisasa nchini kote lakini tiba ya maruhani asilia bado inaendelea kutumiwa na wananchi wengi, wa mijini na vijijini. Pamoja na Tiba ya kiruhani kutumiwa na wananchi wengi, huduma hii imekuwa ikitolewa katika mgumo usio rasmi, hali hii imekuwa ikichangia na kuifanya Tiba ya maruhani, isikubaliwe na watu wengi wasomi na Imani za mapokeo yasiyo ya asili ya mwafrika na mtanzania.
Kwakuwa serikali inatambua umuhimu wa Tiba Asilia hivyo kuanzia mwaka 1961 imekuwa ikichukuwa hatua mbalimbali kwa nia ya kuboresha huduma hiyo kwa kuweka sera, sheria, kanuni, miongozo na mikakati mbalimbali ya uendelezaji na uimalishaji.
Hatua hizo ni pamoja na kuanzisha taasisi za utafiti katika Tiba Asili, kuimalisha huduma za Tiba Asili kwa kuanzishwa kwa kitengo cha Tiba Asili, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Kujuishwa kwa Tiba Asili katika Sera ya Taifa ya Afya yam waka 1990, kutungwa kwa Sheria ya Tiba Asili na Tiba Mbadala Namba 23 ya Mwaka 2002 na Kuanzishwa kwa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala kuanzia Mwaka 2005.
Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala kwa Kushirikiana na Kitengo cha Tiba Asili, Imejikita katika Kutunga kanuni na Kutengeneza miongozo Mbalimbali ikiwa ni pamoja na utaratibu wa kuwasajili waganga na Wakunga wa Tiba Asili nchini ili kuimarisha utekelezaji wa Sheria namba 23 ya mwaka 2002, Sera, kanuni na Miongozo mbalimbali imekwisha sambazwa katika ofisi za waganga wakuu wa mikoa, wilaya,halmashauri za miji na Majiji na mpango wa maendeleo wa Afya ya Msingi wa mwaka  2007 – 2017.Vile vile Wizara imekuwa ikitoa elimu kuhusu Tiba Asili kupitia vyombo vya habari na maonesho ya kitaifa ya Tiba Asili na itaendelea kufanya hivyo.
Ndugu zangu wana Maruhani uhimalishaji wa Tiba Asili unajumuisha:-
·        Usajili wa Waganga, Wakunga na Wauza dawa wa Tiba Asili
·        Uanzishwaji na Usajili wa Vituo rasmi na Vilivyo bora vya kutolea huduma za Tiba Asili na Vinavyokidhi viwango vya Afya.
·        Utafiti na Utengenezaji wa Dawa unaokidhi viwango vya ubora, usalama na uwezo wa Kutibu.
·        Uanzishwaji wa kilimo cha miti dawa ili kuboresha dawa na mazingira.
·        Uwepo wa taratibu za usimamizi na udhibiti wa huduma ya Tiba Asili na Maruhania katika kutoa huduma ya Tiba Asili katika kila halmashauri ya Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji.
Kwahiyo nawaomba kila Mganga wa Maruhania afuate maelezo yaliyotolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia Wazee na Watoto tarehe 15/ januari 2016, juu ya utolewaji wa huduma za Afya kwa Tiba Asili na Tiba Mbadala hapa nchini
hapa nchini kuna Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu za maadili zinazotutaka tuzitii bira shuruti. Ni muhimu kwa kila mtoa huduma ya Afya kwa Tiba Asili ya Maruhani kutoa huduma kwa kuzingatia miongozo ya utoaji wa huduma hizo.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Watu wake wanathamini Tiba Asili na Tiba Mbadala, kwani Tiba Asilia ni Mama wa Tiba ya Kisasa. Sayansi ya Tiba ya Kisasa inatambua sayansi ya Tiba Asilia.
Hata hivyo huduma ya Tiba Asilia na Tiba Mbadala inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na :-
·        kutotambuliwa na baadhi ya watoa huduma wa Tiba za Kisasa kwa sababu mitaala ya mafunzo ya wataalam wa Tiba za Kisasa(Madaktari, wafamasia na Manesi) imewanyima fursa ya kupata maarifa juu ya Tiba Asilia na matumizi yake katika tiba.
·        Katika Jamii pia kumekuwepo na Imani potofu kwa baadhi ya jamii wakihusisha Tiba Asilia na Imani za kishirikina.

·        Ukosekanaji wa fedha za Utafiti umesababisha kukosekana kwa utengenezaji wa dawa zinazokidhi viwango vya ubora, Usalama na Uwezo wa Kutibu na kuzisajiri dawa hizo kwenye mamlaka zinazohusika kwa mujibu wa Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo iliyopo.
·        Uhifadhi mbaya wa mashamba ya Miti dawa ili mitidawa hiyo iweze kufanyiwa utafiti na kuwa dawa bora na salama pamoja na utunzaji endelevu wa mazingira
·        Pia kunachangamoto ya  Uendelezaji wa Wataalam wa Tiba Asili kitaaluma ili wawe na uwezo wa kuboresha huduma zao baada ya kusajiliwa na Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala Kukosekana kwa Muongozo wa ajira za utumishi katika sekta ya Tiba Asili.
Kama tulivyoahidi kuwa tutakuwa na mikutano ya uhamasishaji tunatowa shukurani kwa viongozi wa maruhani kuja kwenye mkutano huu na kujadiliana njia bora ya kufuata maelekezo ya Mhe. Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto juu ya utowaji wa huduma ya Afya kwa Tiba Asili na Tiba Mbadala.
Walimu waambieni Maruhani kuwa Kuna agizo la Serikali linalotakiwa lifuatwe na Viti wao ili viti wao wasije wakapatwa na matatizo ya kisheria yaliyopitishwa katika nchi yetu ya Tanzania katika kutowa huduma ya Tiba Asili pia wafikishieni ujumbe huu watu wote walio na maruhani ambao wanatoa huduma ya Tiba Asili kwa kupitia Maruhani.
Ndugu viongozi wa koo za kiganga na mafundi wake, TRAMEPRO inataka viongozi wa koo za waganga wajitayarishe, tutaendelea na mkutano ya pamoja ili tutambike, ili waganga waliopo katika mila na desturi za kiganga wachukue fomu, kila mila itambike ili waganga wachukuwe fomu na kuanza kufuata utaratibu wa kisheria.
Baadhi ya makundi ya koo za kiganga na watoto wa dawa popote walipo tunataka viongozi wao, Walua, Wabisa, Waswezi, Watongwe, Ruhania, Waganga wa vitabu, Kidama, Kimbunga, Shimbalyoto, Kikola, Ndandi, Matepula, Mbei, lyamite, Shuma, Makamanda, Chambuya, Mchela, Kinyamkela, Lungu Likoko na koo nyingine zote.
Waganga tutowe huduma zetu kwa mfumo wa taasisi na siyo mtu mmoja mmoja kama ilivyo sasa kwa kuanzisha vituo rasmi kwa Mujibu wa Sheria, kanuni na Miongozo, ili iwe rahisi kupata mafunzo yanayostahili kwa huduma tunazozitoa kwa jamii.
Tayarisheni dawa katika sehemu maalum zenye mazingira ya usafi na salama ili kuepuka matumizi ya dawa zinazoweza kuleta madhara pamoja kutunza kumbukumbu kwa kuandika taarifa za ugonjwa na wagonjwa.
Tunaandaa mafunzo ya kuendeleza elimu na taaluma ya Tiba Asili ili mganga awe na uwezo wa kuboresha huduma azitoazo.
Kwa hivi sasa kutakuwa na uratibu wa kila Ngariba wanaotahiri wanaume ili wapate mafunzo maalum ya huduma waitoayo kwa jamii katika kulinda Afya ya Ngaliba mwenyewe na Muhitaji.
Waganga wa Tiba Asili, wauza duka la dawa asili, Wakunga wa Tiba asili, Ngariba wa wanaume, wenye viwanda vidogo vidogo vya utengenezaji wa dawa na wasaidizi wao tujisajiri kwa kipindi hiki cha miezi mitatu (3) na Vijijini tuzingatie miezi sita(6) tuliyopewa ili kuepuka hatua kali za kisheria zitakazo chukuliwa kwa kupuuza kusajiliwa katika kipindi kilichowekwa.
Shirika lenu la dawa asilia na ulinzi wa mazingira (TRAMEPRO) kwa kushirikiana na Watoa huduma wa Tiba Asili kwa ngazi zote , wasimamizi katika ngazi za maamuzi na wadau wote wa Tiba Asili tushirikiane kuitikia wito wa Serikali ili tuweze kupata na kutoa huduma zilizo bora na Salama.
Kwa changamoto zozote zitakazojitokeza katika kipindi cha kutekeleza agizo la Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia Wazee na watoto kwa Tiba Asili na Tiba Mbadala, tuwasiliane ili kupata ufumbuzi wa pamoja kabla ya muda haujamalizika yaani kabla ya Tarehe 15/April, 2016 kwa mjini na tarehe 15/Julai, 2016 kwa vijijini.
Lengo ni Kuona jamii ya watanzania inafikia malengo yake bila kuwepo kwa magonjwa, maisha bora kwaujumla kupitia dawa asilia na mazingira salama na yaliyotunzwa yanayo wazunguka.


ATHUMANI S. UNGANDO
MWENYEKITI, WAMARUHANIA

04/02/ 2016

Monday 10 August 2015

On 00:56 by Unknown   No comments

SERIKALI YAZINDUA KAMATI YA KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA USALAMA ZA WATU WENYE UALBINO

 Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro akiizundua Kamati itakayoshughulikia changamoto za usalama za watu wenye Ualbino nchini kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Kamati hii imeundwa kutokana na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete aliitoa wakati alipokutana na viongozi wa Chama cha Albino nchini (TAS), Machi 5, mwaka huu. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto meza kuu ni Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi, na kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi akiwafafanulia jambo wajumbe wa Kamati itakayoshughulikia changamoto za usalama za watu wenye Ualbino nchini. Kamati hiyo ambayo ni ahadi ya Rais Jakaya Kikwete aliitoa alipokutana na viongozi wa Chama cha Albino nchini (TAS), Machi 5, mwaka huu, imezinduliwa leo na Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro (katikati meza kuu) kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Kulia meza kuu ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.  Mwenyekiti wa Chama cha Albino nchini (TAS), Ernest Kimaya akimshukuru Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro (katikati meza kuu), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (hayupo pichani), Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu (kulia meza kuu), kwa msaada wao ambao umesaidia matukio ya utekaji na mauaji ya albino kupungua kwa kiasi kikubwa. Pia alisema Kamati iliyozinduliwa itaongeza nguvu zaidi katika kukabiliana na changamoto ambazo zinawakabili za usalama wao nchini. Kushoto meza kuu ni Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi. Kamati hiyo ilizinduliwa na Waziri Dk. Migiro kwa niaba ya Waziri Chikawe, katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.   Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro akizungumza na Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi (kulia), na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu mara baada ya kupokelewa Waziri huyo katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ili azindue Kamati itakayoshughulikia changamoto za usalama za watu wenye Ualbino nchini, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Kamati hiyo imeundwa kutokana na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete alipoitoa alipokutana na viongozi wa Chama cha Albino nchini (TAS), Machi 5, mwaka huu. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.  Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro (wanne kulia-mstari wa mbele), Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi (katikati), na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu (watatu kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano wa uzinduzi wa Kamati itakayoshughulikia changamoto za usalama za watu wenye Ualbino nchini. Kamati hiyo ilizinduliwa na Waziri Migiro kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Hata hivyo Kamati hiyo imeundwa kutokana na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete alipoitoa alipokutana na viongozi wa Chama cha Albino nchini (TAS), Machi 5, mwaka huu. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALIWIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Friday 28 November 2014

On 00:34 by Unknown   No comments

Katika swala la utoaji elimu kwa Jamii, elimu juu ya Tiba Asili inafaa itolewe na Waganga wa Asili wenyewe ili kuweza kubadilisha Imani zinazowapotosha wanajamii hata kufikia kutendeana maovu yanayopelekea mauaji. Elimu hii si vyema ikatolewa na Watu wengine kama Vile Maaskofu, Masheikh, Wanasheria, Madaktari wa Kisasa, Wanasiasa n.k kwa kuwa Jamii haitapokea ujumbe wao Kirahisi kwani wamezoeleka kwa Kazi zingine siyo kwa Kazi hiyo ya Imani za ushirikina na uchawi
Katika Imani ya kawaida Kuna Aina za waganga kama ifuatavyo
                              I.            Waganga wa Asili
                           II.            Waganga wa Jadi
                        III.            Waganga wa Kienyeji

1.    WAGANGA WA ASILI.
Mganga wa Asili ni yule anayeshughurika na Tiba za Maradhi kwa Kutumia dawa zaAsili ili kuondoa Maradhi yanayosumbua Jamii iwe kwa Binadamu, wanyama, mimea n.k kwa Kufuata maadili ya utoaji huduma ya Utabibu

2.    WAGANGA WA JADI.
Mganga wa Jadi ni yule anaetumia Mila na Desturi katika Tiba na Utoaji wa dawa kwa wagonjwa iwe Binadamu, Wanyama, Mimea n.k. hivyo hutegemea Zaidi Mila na Desturi kama kanuni na maadili ya utoaji wa Huduma ya Tiba.

3.    MGANGA WA KIENYEJI.
Mganga wa Kienyeji ni Yule Ambaye hana Mafunzo Maalum ya Tiba ya Upande wowote maalum wa tiba  ya Upande wowote katika utoaji wake huduma kwa jamii. Ni mtu anayeweza kuchanganya taaluma mbalimbali hata za kisayansi ili mradi afanikishe alichokusudia. Mganga huyo pia anaweza kutumia vazi lolote liwe la sheikh, askofu, daktari, Mganga wa asili n.k ili mradi atimize alokusudia. Mganga yeyote mwenye fani nzuri akiitumia katika kutenda maovu hufahamika kama mganga wa Kienyeji katika Tiba za Asili.

je Huyu ni Aina gani ya Mganga?

Thursday 27 November 2014

On 01:58 by Unknown   No comments

WATAALAMU WA TIBA ASILI WAKUTANA CHINI YA JUKWAA MOJA; WAONYESHA UMAHIRI KATIKA TIBA ASILI NA MBADALA

Mratibu wa Jukwaa la Tiba Asili Tanzania, Boniventura F. Mwalongo akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja yalikofanyika Maonyesho ya Tiba Asili na Mbadala


Dr. Jumanne wa Huduma ya Uponyaji akimsikiliza mmoja wa waliotembelea Banda lake kwenye Maonyesho ya Tiba za Asili na Mbadala katika Viwanja vya Mnazi Mmoja. Tiba  zinazotolewa na Dk. Jumanne ni zile zinazotokana na Matunda na Mboga Mbalmbali . Simu 0755087303





Dk. Salimu akiwaeleza watu waliofika kwenye maonyesho ya dawa asili jinsi dawa zake zinavyofanya kazi katika viwanja vya Mnazi Mmoja


Dk.Ahmad Darusi Salimu Mkurugenzi wa M. M.D.K Clinic akitoa maelezo ya jinsi dawa zake zinavyotakiwa kutumika. Yeye amebobea katika kutibu Kansa za aina zote na pia anayo dawa inayosaidia kuondoa magonjwa nyemelezi kwa wagonjwa wa UKIMWI. Simu 0754467406, 0787467406

Mkurugenzi wa Kampuniya Dk.Fadhili Herbal Medicine & Nutritional,akitoa maelezo kwa wateja ((hawapo pichani) waliofika kwenye Banda lake wakati wa Maonyesho ya Tiba za Asili na Mbadala yaliyofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja hivi Karibuni.  Dk. Fadhili pia ni Mshauri wa Afya katika Kampuni ya BF SUMA kutoka Marekani inayojishuhulisha na usambazaji wa dawa zenye Virutubisho vinavyoweza kuongeza kinga ya mwili (CD4) kwa 100%, kurekebisha Sukari na zingine nyingi.  Simu 0713834556

Dk. Nyakubaho (katikati) Mkurugenzi wa Kikundi cha tiba Asili cha Nyakiziba Shunga Tradtional Clinic. Wanazo dawa nyingi za kutibu maradhi mbalimbali kama inavyoonekana Pichani. Simu 0784936177, 0755570321

Bi EmilianaKokuhumuliza, Mtabibu wa asili anayetibu kwa kutumia mitishamba kutoka Mkoa wa Kagera. anapatikana Mjini Morogoro. Simu 0766903297. Picha zote na Muchunguzi Kamugisha wa ZUNGU

mhe.Kingunge Ngombale Mwilu akitembelea moja ya mabanda katika maonesho ya kwanza ya kimataifa ya tiba asili ya mwafrika
























































Mkurugenzi wa Kampuni ya Boresa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Tiba Asili Tanzania Tabibu Boniventura Mwalongo akitoa salam za pongezi kumpongeza Mhe. DKT John Pombe Joseph Magufuli kwa Kuchaguliwa Kuwa Raisi wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo tarehe 5 Novemba 2015 katika sherehe za kuapishwa kwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli

kipanya

Popular Posts