Tuesday 21 October 2014

On 14:00 by Unknown   No comments
WASHIRIKI katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Tiba Asili ya Mwafrika yatakayofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Novemba 16 hadi 23 wametakiwa kuonyesha bidhaa bora ambazo zitaleta ushindani katika soko la Tiba Asili.
Maonyesho hayo yanafanyika nchini kwa mara ya kwanza na kuandaliwa na Jukwaa la Tiba Asili Tanzania kushirikiana, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE).
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maonyesho hayo, Boniventure Mwalongo alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa maonyesho hayo yanatoa fursa kwa wadau mbalimbali wa Tiba Asili na Tiba Mbadala kuonyesha bidhaa zenye viwango kama mwanzo wa kupeana changamoto  lakini pia kudhihirisha ubora wa bidhaa za Tiba Asili na Tiba Mbadala.
“Tunaka kuona bidhaa zenye ubora kuanzia katika ufungashaji, maelekezo sahihi kuhusu matumizi lakini pia bidhaa hizo ziwe zinafaa kwa matumizi ya binadamu ikiwa ni pamoja na kuwa na viwango vinavyotakiwa,” alisema Mwalongo.
Mwalongo alichukua fursa hiyo kuwaomba Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala kutoa taarifa ya maonyesho hayo kwa waratibu wa mikoa na wilaya ili nao waweze kuwataarifu watabibu wa Tiba Asili na Mbadala waliosajiliwa katika maeneo yao ili waweze kushiriki kirahisi katika maonyesho hayo.
“Njia hii itakuwa bora zaidi kwasababu itawarahishishia washiriki kupata fomu kutoka kwa waratibu wao wa wilaya au mkoa ambao pia wanawatambua kisheria,” alisema Mwalongo.
Washiriki katika maonyesho hayo ni pamoja na Watabibu wa Tiba Asili, Watengenezaji wa Dawa Asili, Wakunga wa Tiba Asili, Kampuni za Dawa Asili na vipodozi vya dawa asili, Wasambazaji wa Vifaa vya Tiba Asili na Tiba Mbadala, Watengenezaji wa vyakula asili, kliniki za tiba asili na Tiba Mbadala.
Aidha kuna taratibu nyingine za kuyashirikisha mashirika mengine ya kibiashara, taasisi binafsi za za serikali ili kutoa nafasi ya kutangaza biashara zao kupitia maonyesho hayo ambayo yatashirikisha wadau wa Tida Asili na Tiba Mbadala kutoka ndani na nje ya nchi.
Kwa mujibu wa Mwalongo, hadi sasa kuna baadhi ya kampuni na taasisi ambazo zimeonyesha mwelekeo wa kutaka kudhamini maonyesho hayo na kuwa taarifa rasmi itatolewa baada ya kufikia makubaliano.
Mbali na kutangaza Tiba Mbadala na Tiba Asili kwa mapana yake, Mwalongo alisema kuwa wanataka kujenga mtandao mkubwa wa kibiashara katika huduma ya Tiba Asili na Tiba Mbadala kwa nchi za Afrika.

0 comments:

Post a Comment

Mkurugenzi wa Kampuni ya Boresa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Tiba Asili Tanzania Tabibu Boniventura Mwalongo akitoa salam za pongezi kumpongeza Mhe. DKT John Pombe Joseph Magufuli kwa Kuchaguliwa Kuwa Raisi wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo tarehe 5 Novemba 2015 katika sherehe za kuapishwa kwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli

kipanya

Popular Posts