Saturday 6 February 2016

On 03:16 by Unknown   No comments

·        Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa
·        Afisa Maendeleo wa Mtaa
·        Mwenyekiti wa Kamati ya Afya na Mazingira
·        Wajumbe wa Serikali ya Mtaa
·        Mwenyekiti wa Maruhania
·        Katibu wa Maruhania
·        Waganga Mafundi, Walimu wa Maruhania (Watabibu wa Tiba Asilia)
·        Mabibi na Mabwana.
Habari za Muda huu
Leo ni siku ya pekee kwa wanamaruhania na watu wote wanaopenda maendeleo yetu na hasa katika tiba asilia na afya ya watanzania. Ni siku ambayo tunaandika historia katika Tiba Asilia na Maruhania. Kihistoria hakuna anayefahamu kwa hakika lini ushirikiano kati ya mwanadamu na Maruhani katika kutoa huduma ya Tiba Asilia na ilianza lini kutumika hapa kwetu Tanzania ila kila mmoja wetu atakubariana kuwa ilianza tuu pale binadamu wa kwanza alipoanza kuishi katika nchi yetu kwa miaka yote ya kuwepo kwa binadamu hapa Tanzania, Tiba ya kiruhani nayo imekuwa muhimili wa matibabu ya Tiba Asili.
Pamoja na kuwepo kwa maendeleo makubwa katika teknolojia na usambazaji wa huduma ya Tiba ya kisasa nchini kote lakini tiba ya maruhani asilia bado inaendelea kutumiwa na wananchi wengi, wa mijini na vijijini. Pamoja na Tiba ya kiruhani kutumiwa na wananchi wengi, huduma hii imekuwa ikitolewa katika mgumo usio rasmi, hali hii imekuwa ikichangia na kuifanya Tiba ya maruhani, isikubaliwe na watu wengi wasomi na Imani za mapokeo yasiyo ya asili ya mwafrika na mtanzania.
Kwakuwa serikali inatambua umuhimu wa Tiba Asilia hivyo kuanzia mwaka 1961 imekuwa ikichukuwa hatua mbalimbali kwa nia ya kuboresha huduma hiyo kwa kuweka sera, sheria, kanuni, miongozo na mikakati mbalimbali ya uendelezaji na uimalishaji.
Hatua hizo ni pamoja na kuanzisha taasisi za utafiti katika Tiba Asili, kuimalisha huduma za Tiba Asili kwa kuanzishwa kwa kitengo cha Tiba Asili, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Kujuishwa kwa Tiba Asili katika Sera ya Taifa ya Afya yam waka 1990, kutungwa kwa Sheria ya Tiba Asili na Tiba Mbadala Namba 23 ya Mwaka 2002 na Kuanzishwa kwa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala kuanzia Mwaka 2005.
Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala kwa Kushirikiana na Kitengo cha Tiba Asili, Imejikita katika Kutunga kanuni na Kutengeneza miongozo Mbalimbali ikiwa ni pamoja na utaratibu wa kuwasajili waganga na Wakunga wa Tiba Asili nchini ili kuimarisha utekelezaji wa Sheria namba 23 ya mwaka 2002, Sera, kanuni na Miongozo mbalimbali imekwisha sambazwa katika ofisi za waganga wakuu wa mikoa, wilaya,halmashauri za miji na Majiji na mpango wa maendeleo wa Afya ya Msingi wa mwaka  2007 – 2017.Vile vile Wizara imekuwa ikitoa elimu kuhusu Tiba Asili kupitia vyombo vya habari na maonesho ya kitaifa ya Tiba Asili na itaendelea kufanya hivyo.
Ndugu zangu wana Maruhani uhimalishaji wa Tiba Asili unajumuisha:-
·        Usajili wa Waganga, Wakunga na Wauza dawa wa Tiba Asili
·        Uanzishwaji na Usajili wa Vituo rasmi na Vilivyo bora vya kutolea huduma za Tiba Asili na Vinavyokidhi viwango vya Afya.
·        Utafiti na Utengenezaji wa Dawa unaokidhi viwango vya ubora, usalama na uwezo wa Kutibu.
·        Uanzishwaji wa kilimo cha miti dawa ili kuboresha dawa na mazingira.
·        Uwepo wa taratibu za usimamizi na udhibiti wa huduma ya Tiba Asili na Maruhania katika kutoa huduma ya Tiba Asili katika kila halmashauri ya Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji.
Kwahiyo nawaomba kila Mganga wa Maruhania afuate maelezo yaliyotolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia Wazee na Watoto tarehe 15/ januari 2016, juu ya utolewaji wa huduma za Afya kwa Tiba Asili na Tiba Mbadala hapa nchini
hapa nchini kuna Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu za maadili zinazotutaka tuzitii bira shuruti. Ni muhimu kwa kila mtoa huduma ya Afya kwa Tiba Asili ya Maruhani kutoa huduma kwa kuzingatia miongozo ya utoaji wa huduma hizo.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Watu wake wanathamini Tiba Asili na Tiba Mbadala, kwani Tiba Asilia ni Mama wa Tiba ya Kisasa. Sayansi ya Tiba ya Kisasa inatambua sayansi ya Tiba Asilia.
Hata hivyo huduma ya Tiba Asilia na Tiba Mbadala inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na :-
·        kutotambuliwa na baadhi ya watoa huduma wa Tiba za Kisasa kwa sababu mitaala ya mafunzo ya wataalam wa Tiba za Kisasa(Madaktari, wafamasia na Manesi) imewanyima fursa ya kupata maarifa juu ya Tiba Asilia na matumizi yake katika tiba.
·        Katika Jamii pia kumekuwepo na Imani potofu kwa baadhi ya jamii wakihusisha Tiba Asilia na Imani za kishirikina.

·        Ukosekanaji wa fedha za Utafiti umesababisha kukosekana kwa utengenezaji wa dawa zinazokidhi viwango vya ubora, Usalama na Uwezo wa Kutibu na kuzisajiri dawa hizo kwenye mamlaka zinazohusika kwa mujibu wa Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo iliyopo.
·        Uhifadhi mbaya wa mashamba ya Miti dawa ili mitidawa hiyo iweze kufanyiwa utafiti na kuwa dawa bora na salama pamoja na utunzaji endelevu wa mazingira
·        Pia kunachangamoto ya  Uendelezaji wa Wataalam wa Tiba Asili kitaaluma ili wawe na uwezo wa kuboresha huduma zao baada ya kusajiliwa na Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala Kukosekana kwa Muongozo wa ajira za utumishi katika sekta ya Tiba Asili.
Kama tulivyoahidi kuwa tutakuwa na mikutano ya uhamasishaji tunatowa shukurani kwa viongozi wa maruhani kuja kwenye mkutano huu na kujadiliana njia bora ya kufuata maelekezo ya Mhe. Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto juu ya utowaji wa huduma ya Afya kwa Tiba Asili na Tiba Mbadala.
Walimu waambieni Maruhani kuwa Kuna agizo la Serikali linalotakiwa lifuatwe na Viti wao ili viti wao wasije wakapatwa na matatizo ya kisheria yaliyopitishwa katika nchi yetu ya Tanzania katika kutowa huduma ya Tiba Asili pia wafikishieni ujumbe huu watu wote walio na maruhani ambao wanatoa huduma ya Tiba Asili kwa kupitia Maruhani.
Ndugu viongozi wa koo za kiganga na mafundi wake, TRAMEPRO inataka viongozi wa koo za waganga wajitayarishe, tutaendelea na mkutano ya pamoja ili tutambike, ili waganga waliopo katika mila na desturi za kiganga wachukue fomu, kila mila itambike ili waganga wachukuwe fomu na kuanza kufuata utaratibu wa kisheria.
Baadhi ya makundi ya koo za kiganga na watoto wa dawa popote walipo tunataka viongozi wao, Walua, Wabisa, Waswezi, Watongwe, Ruhania, Waganga wa vitabu, Kidama, Kimbunga, Shimbalyoto, Kikola, Ndandi, Matepula, Mbei, lyamite, Shuma, Makamanda, Chambuya, Mchela, Kinyamkela, Lungu Likoko na koo nyingine zote.
Waganga tutowe huduma zetu kwa mfumo wa taasisi na siyo mtu mmoja mmoja kama ilivyo sasa kwa kuanzisha vituo rasmi kwa Mujibu wa Sheria, kanuni na Miongozo, ili iwe rahisi kupata mafunzo yanayostahili kwa huduma tunazozitoa kwa jamii.
Tayarisheni dawa katika sehemu maalum zenye mazingira ya usafi na salama ili kuepuka matumizi ya dawa zinazoweza kuleta madhara pamoja kutunza kumbukumbu kwa kuandika taarifa za ugonjwa na wagonjwa.
Tunaandaa mafunzo ya kuendeleza elimu na taaluma ya Tiba Asili ili mganga awe na uwezo wa kuboresha huduma azitoazo.
Kwa hivi sasa kutakuwa na uratibu wa kila Ngariba wanaotahiri wanaume ili wapate mafunzo maalum ya huduma waitoayo kwa jamii katika kulinda Afya ya Ngaliba mwenyewe na Muhitaji.
Waganga wa Tiba Asili, wauza duka la dawa asili, Wakunga wa Tiba asili, Ngariba wa wanaume, wenye viwanda vidogo vidogo vya utengenezaji wa dawa na wasaidizi wao tujisajiri kwa kipindi hiki cha miezi mitatu (3) na Vijijini tuzingatie miezi sita(6) tuliyopewa ili kuepuka hatua kali za kisheria zitakazo chukuliwa kwa kupuuza kusajiliwa katika kipindi kilichowekwa.
Shirika lenu la dawa asilia na ulinzi wa mazingira (TRAMEPRO) kwa kushirikiana na Watoa huduma wa Tiba Asili kwa ngazi zote , wasimamizi katika ngazi za maamuzi na wadau wote wa Tiba Asili tushirikiane kuitikia wito wa Serikali ili tuweze kupata na kutoa huduma zilizo bora na Salama.
Kwa changamoto zozote zitakazojitokeza katika kipindi cha kutekeleza agizo la Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia Wazee na watoto kwa Tiba Asili na Tiba Mbadala, tuwasiliane ili kupata ufumbuzi wa pamoja kabla ya muda haujamalizika yaani kabla ya Tarehe 15/April, 2016 kwa mjini na tarehe 15/Julai, 2016 kwa vijijini.
Lengo ni Kuona jamii ya watanzania inafikia malengo yake bila kuwepo kwa magonjwa, maisha bora kwaujumla kupitia dawa asilia na mazingira salama na yaliyotunzwa yanayo wazunguka.


ATHUMANI S. UNGANDO
MWENYEKITI, WAMARUHANIA

04/02/ 2016

0 comments:

Post a Comment

Mkurugenzi wa Kampuni ya Boresa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Tiba Asili Tanzania Tabibu Boniventura Mwalongo akitoa salam za pongezi kumpongeza Mhe. DKT John Pombe Joseph Magufuli kwa Kuchaguliwa Kuwa Raisi wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo tarehe 5 Novemba 2015 katika sherehe za kuapishwa kwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli

kipanya

Popular Posts