Monday 7 July 2014

On 05:01 by Unknown   No comments
WATABIBU wa tiba za asili mkoani Mbeya wamelaani vikali kitendo cha baadhi ya watabibu na waganga kujihusisha na ushirikina na hasa tukio lililotokea jijini  Mwanza kwa wanga wa kienyeji kufanya vitendo vya ajabu na kutaka visijirudie.
Hayo yamebainishwa na watabibu wa tiba za asili Juzi wakati wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari kutoa tamko la kulaani vitendo vya ajabu vinavyofanywa na waganga wa jadi na kusababisha uvunjifu wa amani. 
Mratibu wa taasisi ya watabibu wa tiba za asili Tanzania (ATME) mkoa wa Mbeya, Boniventure Mwalongo, alisema kuwa  wanalaani vikali vitendo vya kikatili vinavyofanywa na waganga wa tiba za asili.
“Nashukuru viongozi wa vyama vya watoatiba za asili mkoa wa Mbeya, kwa ushirikiano wenu na kukutana kwa pamoja kulaani vitendo vibaya vilivyo fanywa na waganga wa jadi wawili jijini
Mwanza vya kikatili na hatimaye kukutwa na mikino ya binadamu,” Alisema Mwalongo
Alisema kuwa vitendo hivyo havikubaliki na wanapinga vikali na hawataki vikatokea mkoani Mbeya kwani ni aibu kwa taaluma yao ya utabibu.
Kwa upande wa washiliki ambao ni viongozi wa watabibu mkoa wa Mbeya wamesema kuwa vitendo hivyo havi fai kutokea na watabibu na wakunga wa jadi wanalaani na wanaomba sheria kali zichukuliwe kwa wale watakao kamatwa wakijihusisha na ukalili wa aina hiyo.
Mmoja wa watabibu hao, Addala Azizi alisema kuwa wao kama watoa tiba za asili wa mkoa wa Mbeya wanalaani vitendo vya aina hiyo visijirudie mahali popote Tanzania na hawapendi vitokee.
 
Nae Zahara Masudi alisema kuwa tatizo limekuwa ni kwa wateja na sio kwa waganda wa jadi kwani ndio wanao washawili kufanya vitendo hivyo.
Alisema kuwa binadamu tunazalilika kwa kufikili mambo ya ajabu na tunayo yafanya hasa wale wanao kuwa na ufinyu wa kufikili na kuwaza kuwa wanaweza kupata utajili ama kupona baada ya kumuua mtu mwingine huo ni upungufu wa akili.
Serikali itunge sheria kali kwaajili ya kuwabana watakao kamatwa wakijihusisha na mambo ya ajabu na kufanya matukio ya kishirikina.
Watabibu hao walikutana baada ya kutokea tukio la ajabu lililotokea mkoani mwanza mwishoni mwa mwezi uliopita la mganga wa jadi kudaiwa kukutwa na kiganja cha mkono wa binadamu.

0 comments:

Post a Comment

Mkurugenzi wa Kampuni ya Boresa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Tiba Asili Tanzania Tabibu Boniventura Mwalongo akitoa salam za pongezi kumpongeza Mhe. DKT John Pombe Joseph Magufuli kwa Kuchaguliwa Kuwa Raisi wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo tarehe 5 Novemba 2015 katika sherehe za kuapishwa kwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli

kipanya

Popular Posts