
Waziri
wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro akiizundua Kamati
itakayoshughulikia changamoto za usalama za watu wenye Ualbino nchini
kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Kamati
hii imeundwa kutokana na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete aliitoa wakati
alipokutana na viongozi wa Chama cha Albino nchini (TAS), Machi 5, mwaka
huu. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto meza kuu ni
Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi, na
kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu. Picha zote na
Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Kaimu
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi
akiwafafanulia jambo wajumbe wa Kamati itakayoshughulikia changamoto za
usalama za watu wenye Ualbino nchini. Kamati hiyo ambayo ni ahadi ya
Rais Jakaya Kikwete aliitoa alipokutana na viongozi wa Chama cha Albino
nchini (TAS), Machi 5, mwaka huu, imezinduliwa leo na Waziri wa Sheria
na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro (katikati meza kuu) kwa niaba ya Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Uzinduzi huo ulifanyika
katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini
Dar es Salaam leo. Kulia meza kuu ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP
Ernest Mangu. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.

Mwenyekiti
wa Chama cha Albino nchini (TAS), Ernest Kimaya akimshukuru Waziri wa
Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro (katikati meza kuu), Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (hayupo pichani), Mkuu wa Jeshi
la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu (kulia meza kuu), kwa msaada wao
ambao umesaidia matukio ya utekaji na mauaji ya albino kupungua kwa
kiasi kikubwa. Pia alisema Kamati iliyozinduliwa itaongeza nguvu zaidi
katika kukabiliana na changamoto ambazo zinawakabili za usalama wao
nchini. Kushoto meza kuu ni Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi, Haji Janabi. Kamati hiyo ilizinduliwa na Waziri Dk. Migiro kwa
niaba ya Waziri Chikawe, katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri
wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro akizungumza na Kaimu Katibu
Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi (kulia), na Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu mara baada ya kupokelewa Waziri
huyo katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ili azindue
Kamati itakayoshughulikia changamoto za usalama za watu wenye Ualbino
nchini, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe.
Kamati hiyo imeundwa kutokana na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete alipoitoa
alipokutana na viongozi wa Chama cha Albino nchini (TAS), Machi 5, mwaka
huu. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix
Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri
wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro (wanne kulia-mstari wa
mbele), Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi
(katikati), na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu (watatu
kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano wa uzinduzi
wa Kamati itakayoshughulikia changamoto za usalama za watu wenye Ualbino
nchini. Kamati hiyo ilizinduliwa na Waziri Migiro kwa niaba ya Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Hata hivyo Kamati hiyo
imeundwa kutokana na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete alipoitoa alipokutana
na viongozi wa Chama cha Albino nchini (TAS), Machi 5, mwaka huu.
Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Felix Mwagara,
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALIWIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
0 comments:
Post a Comment