Saturday, 6 February 2016
On 03:16 by Unknown No comments
·
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa
·
Afisa Maendeleo wa Mtaa
·
Mwenyekiti wa Kamati ya Afya na Mazingira
·
Wajumbe wa Serikali ya Mtaa
·
Mwenyekiti wa Maruhania
·
Katibu wa Maruhania
·
Waganga Mafundi, Walimu wa Maruhania (Watabibu wa Tiba
Asilia)
·
Mabibi na Mabwana.
Habari za Muda huu
Leo
ni siku ya pekee kwa wanamaruhania na watu wote wanaopenda maendeleo yetu na
hasa katika tiba asilia na afya ya watanzania. Ni siku ambayo tunaandika
historia katika Tiba Asilia na Maruhania. Kihistoria hakuna anayefahamu kwa
hakika lini ushirikiano kati ya mwanadamu na Maruhani katika kutoa huduma ya
Tiba Asilia na ilianza lini kutumika hapa kwetu Tanzania ila kila mmoja wetu
atakubariana kuwa ilianza tuu pale binadamu wa kwanza alipoanza kuishi katika
nchi yetu kwa miaka yote ya kuwepo kwa binadamu hapa Tanzania, Tiba ya kiruhani
nayo imekuwa muhimili wa matibabu ya Tiba Asili.
Pamoja
na kuwepo kwa maendeleo makubwa katika teknolojia na usambazaji wa huduma ya
Tiba ya kisasa nchini kote lakini tiba ya maruhani asilia bado inaendelea
kutumiwa na wananchi wengi, wa mijini na vijijini. Pamoja na Tiba ya kiruhani
kutumiwa na wananchi wengi, huduma hii imekuwa ikitolewa katika mgumo usio
rasmi, hali hii imekuwa ikichangia na kuifanya Tiba ya maruhani, isikubaliwe na
watu wengi wasomi na Imani za mapokeo yasiyo ya asili ya mwafrika na mtanzania.
Kwakuwa
serikali inatambua umuhimu wa Tiba Asilia hivyo kuanzia mwaka 1961 imekuwa
ikichukuwa hatua mbalimbali kwa nia ya kuboresha huduma hiyo kwa kuweka sera,
sheria, kanuni, miongozo na mikakati mbalimbali ya uendelezaji na uimalishaji.
Hatua
hizo ni pamoja na kuanzisha taasisi za utafiti katika Tiba Asili, kuimalisha
huduma za Tiba Asili kwa kuanzishwa kwa kitengo cha Tiba Asili, Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Kujuishwa kwa Tiba Asili katika
Sera ya Taifa ya Afya yam waka 1990, kutungwa kwa Sheria ya Tiba Asili na Tiba
Mbadala Namba 23 ya Mwaka 2002 na Kuanzishwa kwa Baraza la Tiba Asili na Tiba
Mbadala kuanzia Mwaka 2005.
Baraza
la Tiba Asili na Tiba Mbadala kwa Kushirikiana na Kitengo cha Tiba Asili,
Imejikita katika Kutunga kanuni na Kutengeneza miongozo Mbalimbali ikiwa ni
pamoja na utaratibu wa kuwasajili waganga na Wakunga wa Tiba Asili nchini ili
kuimarisha utekelezaji wa Sheria namba 23 ya mwaka 2002, Sera, kanuni na
Miongozo mbalimbali imekwisha sambazwa katika ofisi za waganga wakuu wa mikoa,
wilaya,halmashauri za miji na Majiji na mpango wa maendeleo wa Afya ya Msingi
wa mwaka 2007 – 2017.Vile vile Wizara
imekuwa ikitoa elimu kuhusu Tiba Asili kupitia vyombo vya habari na maonesho ya
kitaifa ya Tiba Asili na itaendelea kufanya hivyo.
Ndugu
zangu wana Maruhani uhimalishaji wa Tiba Asili unajumuisha:-
·
Usajili wa Waganga,
Wakunga na Wauza dawa wa Tiba Asili
·
Uanzishwaji na Usajili
wa Vituo rasmi na Vilivyo bora vya kutolea huduma za Tiba Asili na Vinavyokidhi
viwango vya Afya.
·
Utafiti na
Utengenezaji wa Dawa unaokidhi viwango vya ubora, usalama na uwezo wa Kutibu.
·
Uanzishwaji wa kilimo
cha miti dawa ili kuboresha dawa na mazingira.
·
Uwepo wa taratibu za
usimamizi na udhibiti wa huduma ya Tiba Asili na Maruhania katika kutoa huduma
ya Tiba Asili katika kila halmashauri ya Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji.
Kwahiyo
nawaomba kila Mganga wa Maruhania afuate maelezo yaliyotolewa na Waziri wa
Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia Wazee na Watoto tarehe 15/ januari 2016, juu
ya utolewaji wa huduma za Afya kwa Tiba Asili na Tiba Mbadala hapa nchini
hapa
nchini kuna Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu za maadili zinazotutaka tuzitii
bira shuruti. Ni muhimu kwa kila mtoa huduma ya Afya kwa Tiba Asili ya Maruhani
kutoa huduma kwa kuzingatia miongozo ya utoaji wa huduma hizo.
Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na Watu wake wanathamini Tiba Asili na Tiba Mbadala, kwani
Tiba Asilia ni Mama wa Tiba ya Kisasa. Sayansi ya Tiba ya Kisasa inatambua
sayansi ya Tiba Asilia.
Hata
hivyo huduma ya Tiba Asilia na Tiba Mbadala inakabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwa ni pamoja na :-
·
kutotambuliwa na
baadhi ya watoa huduma wa Tiba za Kisasa kwa sababu mitaala ya mafunzo ya
wataalam wa Tiba za Kisasa(Madaktari, wafamasia na Manesi) imewanyima fursa ya
kupata maarifa juu ya Tiba Asilia na matumizi yake katika tiba.
·
Katika Jamii pia
kumekuwepo na Imani potofu kwa baadhi ya jamii wakihusisha Tiba Asilia na Imani
za kishirikina.
·
Ukosekanaji wa fedha
za Utafiti umesababisha kukosekana kwa utengenezaji wa dawa zinazokidhi viwango
vya ubora, Usalama na Uwezo wa Kutibu na kuzisajiri dawa hizo kwenye mamlaka
zinazohusika kwa mujibu wa Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo iliyopo.
·
Uhifadhi mbaya wa
mashamba ya Miti dawa ili mitidawa hiyo iweze kufanyiwa utafiti na kuwa dawa
bora na salama pamoja na utunzaji endelevu wa mazingira
·
Pia kunachangamoto
ya Uendelezaji wa Wataalam wa Tiba Asili
kitaaluma ili wawe na uwezo wa kuboresha huduma zao baada ya kusajiliwa na
Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala Kukosekana kwa Muongozo wa ajira za
utumishi katika sekta ya Tiba Asili.
Kama
tulivyoahidi kuwa tutakuwa na mikutano ya uhamasishaji tunatowa shukurani kwa
viongozi wa maruhani kuja kwenye mkutano huu na kujadiliana njia bora ya
kufuata maelekezo ya Mhe. Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na
Watoto juu ya utowaji wa huduma ya Afya kwa Tiba Asili na Tiba Mbadala.
Walimu
waambieni Maruhani kuwa Kuna agizo la Serikali linalotakiwa lifuatwe na Viti
wao ili viti wao wasije wakapatwa na matatizo ya kisheria yaliyopitishwa katika
nchi yetu ya Tanzania katika kutowa huduma ya Tiba Asili pia wafikishieni
ujumbe huu watu wote walio na maruhani ambao wanatoa huduma ya Tiba Asili kwa
kupitia Maruhani.
Ndugu
viongozi wa koo za kiganga na mafundi wake, TRAMEPRO inataka viongozi wa koo za
waganga wajitayarishe, tutaendelea na mkutano ya pamoja ili tutambike, ili
waganga waliopo katika mila na desturi za kiganga wachukue fomu, kila mila
itambike ili waganga wachukuwe fomu na kuanza kufuata utaratibu wa kisheria.
Baadhi
ya makundi ya koo za kiganga na watoto wa dawa popote walipo tunataka viongozi
wao, Walua, Wabisa, Waswezi, Watongwe, Ruhania, Waganga wa vitabu, Kidama, Kimbunga,
Shimbalyoto, Kikola, Ndandi, Matepula, Mbei, lyamite, Shuma, Makamanda,
Chambuya, Mchela, Kinyamkela, Lungu Likoko na koo nyingine zote.
Waganga
tutowe huduma zetu kwa mfumo wa taasisi na siyo mtu mmoja mmoja kama ilivyo
sasa kwa kuanzisha vituo rasmi kwa Mujibu wa Sheria, kanuni na Miongozo, ili
iwe rahisi kupata mafunzo yanayostahili kwa huduma tunazozitoa kwa jamii.
Tayarisheni
dawa katika sehemu maalum zenye mazingira ya usafi na salama ili kuepuka
matumizi ya dawa zinazoweza kuleta madhara pamoja kutunza kumbukumbu kwa
kuandika taarifa za ugonjwa na wagonjwa.
Tunaandaa
mafunzo ya kuendeleza elimu na taaluma ya Tiba Asili ili mganga awe na uwezo wa
kuboresha huduma azitoazo.
Kwa
hivi sasa kutakuwa na uratibu wa kila Ngariba wanaotahiri wanaume ili wapate
mafunzo maalum ya huduma waitoayo kwa jamii katika kulinda Afya ya Ngaliba
mwenyewe na Muhitaji.
Waganga
wa Tiba Asili, wauza duka la dawa asili, Wakunga wa Tiba asili, Ngariba wa
wanaume, wenye viwanda vidogo vidogo vya utengenezaji wa dawa na wasaidizi wao
tujisajiri kwa kipindi hiki cha miezi mitatu (3) na Vijijini tuzingatie miezi
sita(6) tuliyopewa ili kuepuka hatua kali za kisheria zitakazo chukuliwa kwa
kupuuza kusajiliwa katika kipindi kilichowekwa.
Shirika
lenu la dawa asilia na ulinzi wa mazingira (TRAMEPRO) kwa kushirikiana na Watoa
huduma wa Tiba Asili kwa ngazi zote , wasimamizi katika ngazi za maamuzi na
wadau wote wa Tiba Asili tushirikiane kuitikia wito wa Serikali ili tuweze
kupata na kutoa huduma zilizo bora na Salama.
Kwa changamoto zozote zitakazojitokeza
katika kipindi cha kutekeleza agizo la Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
jinsia Wazee na watoto kwa Tiba Asili na Tiba Mbadala, tuwasiliane ili kupata
ufumbuzi wa pamoja kabla ya muda haujamalizika yaani kabla ya Tarehe 15/April,
2016 kwa mjini na tarehe 15/Julai, 2016 kwa vijijini.
Lengo
ni Kuona jamii ya watanzania inafikia malengo yake bila kuwepo kwa magonjwa,
maisha bora kwaujumla kupitia dawa asilia na mazingira salama na yaliyotunzwa
yanayo wazunguka.
ATHUMANI S. UNGANDO
MWENYEKITI, WAMARUHANIA
04/02/
2016
Monday, 10 August 2015
On 00:56 by Unknown No comments
Waziri
wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro akiizundua Kamati
itakayoshughulikia changamoto za usalama za watu wenye Ualbino nchini
kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Kamati
hii imeundwa kutokana na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete aliitoa wakati
alipokutana na viongozi wa Chama cha Albino nchini (TAS), Machi 5, mwaka
huu. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto meza kuu ni
Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi, na
kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu. Picha zote na
Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi akiwafafanulia jambo wajumbe wa Kamati itakayoshughulikia changamoto za usalama za watu wenye Ualbino nchini. Kamati hiyo ambayo ni ahadi ya Rais Jakaya Kikwete aliitoa alipokutana na viongozi wa Chama cha Albino nchini (TAS), Machi 5, mwaka huu, imezinduliwa leo na Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro (katikati meza kuu) kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Kulia meza kuu ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Mwenyekiti wa Chama cha Albino nchini (TAS), Ernest Kimaya akimshukuru Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro (katikati meza kuu), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (hayupo pichani), Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu (kulia meza kuu), kwa msaada wao ambao umesaidia matukio ya utekaji na mauaji ya albino kupungua kwa kiasi kikubwa. Pia alisema Kamati iliyozinduliwa itaongeza nguvu zaidi katika kukabiliana na changamoto ambazo zinawakabili za usalama wao nchini. Kushoto meza kuu ni Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi. Kamati hiyo ilizinduliwa na Waziri Dk. Migiro kwa niaba ya Waziri Chikawe, katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro akizungumza na Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi (kulia), na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu mara baada ya kupokelewa Waziri huyo katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ili azindue Kamati itakayoshughulikia changamoto za usalama za watu wenye Ualbino nchini, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Kamati hiyo imeundwa kutokana na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete alipoitoa alipokutana na viongozi wa Chama cha Albino nchini (TAS), Machi 5, mwaka huu. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro (wanne kulia-mstari wa mbele), Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi (katikati), na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu (watatu kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano wa uzinduzi wa Kamati itakayoshughulikia changamoto za usalama za watu wenye Ualbino nchini. Kamati hiyo ilizinduliwa na Waziri Migiro kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Hata hivyo Kamati hiyo imeundwa kutokana na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete alipoitoa alipokutana na viongozi wa Chama cha Albino nchini (TAS), Machi 5, mwaka huu. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALIWIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Friday, 28 November 2014
On 00:34 by Unknown No comments
Katika swala la utoaji elimu kwa Jamii, elimu juu ya Tiba
Asili inafaa itolewe na Waganga wa Asili wenyewe ili kuweza kubadilisha Imani
zinazowapotosha wanajamii hata kufikia kutendeana maovu yanayopelekea mauaji. Elimu
hii si vyema ikatolewa na Watu wengine kama Vile Maaskofu, Masheikh,
Wanasheria, Madaktari wa Kisasa, Wanasiasa n.k kwa kuwa Jamii haitapokea ujumbe
wao Kirahisi kwani wamezoeleka kwa Kazi zingine siyo kwa Kazi hiyo ya Imani za
ushirikina na uchawi
Katika Imani ya kawaida
Kuna Aina za waganga kama ifuatavyo
I.
Waganga wa Asili
II.
Waganga wa Jadi
III.
Waganga wa Kienyeji
1.
WAGANGA WA ASILI.
Mganga wa Asili ni yule anayeshughurika na Tiba za Maradhi kwa Kutumia
dawa zaAsili ili kuondoa Maradhi yanayosumbua Jamii iwe kwa Binadamu, wanyama,
mimea n.k kwa Kufuata maadili ya utoaji huduma ya Utabibu
2.
WAGANGA WA JADI.
Mganga wa Jadi ni yule anaetumia Mila na Desturi katika Tiba na Utoaji wa
dawa kwa wagonjwa iwe Binadamu, Wanyama, Mimea n.k. hivyo hutegemea Zaidi Mila
na Desturi kama kanuni na maadili ya utoaji wa Huduma ya Tiba.
3.
MGANGA WA KIENYEJI.
Mganga wa Kienyeji ni Yule Ambaye hana Mafunzo Maalum
ya Tiba ya Upande wowote maalum wa tiba
ya Upande wowote katika utoaji wake huduma kwa jamii. Ni mtu anayeweza
kuchanganya taaluma mbalimbali hata za kisayansi ili mradi afanikishe
alichokusudia. Mganga huyo pia anaweza kutumia vazi lolote liwe la sheikh,
askofu, daktari, Mganga wa asili n.k ili mradi atimize alokusudia. Mganga
yeyote mwenye fani nzuri akiitumia katika kutenda maovu hufahamika kama mganga
wa Kienyeji katika Tiba za Asili.
Thursday, 27 November 2014
On 01:58 by Unknown No comments
WATAALAMU WA TIBA ASILI WAKUTANA CHINI YA JUKWAA MOJA; WAONYESHA UMAHIRI KATIKA TIBA ASILI NA MBADALA
Dk. Salimu akiwaeleza watu waliofika kwenye maonyesho ya dawa asili jinsi dawa zake zinavyofanya kazi katika viwanja vya Mnazi Mmoja |
Subscribe to:
Posts (Atom)
Mkurugenzi wa Kampuni ya Boresa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Tiba Asili Tanzania Tabibu Boniventura Mwalongo akitoa salam za pongezi kumpongeza Mhe. DKT John Pombe Joseph Magufuli kwa Kuchaguliwa Kuwa Raisi wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo tarehe 5 Novemba 2015 katika sherehe za kuapishwa kwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
kipanya
Popular Posts
-
TUJIKUMBUSHE YALE MAAJABU SABA YA DUNIA YA MWAKA 2007 Na Alberto sanga endelea...
-
habari zilizotufikia,Samaki huyu adimu kabisa duniani kumtia machoni ameonekana amefariki ama amekufa pembeni mwa ufukwe wa baha...
-
WAGANGA na wakunga wa tiba asili ni miongoni mwa watoa huduma za afya mbadala nchini ambapo wanaongozwa na sheria, mila, desturi na tarati...
-
WATAALAMU WA TIBA ASILI WAKUTANA CHINI YA JUKWAA MOJA; WAONYESHA UMAHIRI KATIKA TIBA ASILI NA MBADALA Mratibu wa Jukwaa la Tiba Asil...
-
FAHAMU KUHUSU TIBA A SILIA YA KUUNGANISHA MIFUPA Watu wengi wanao pata ajali za barabarani na kuvunjika viungo ...
-
WASHIRIKI katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Tiba Asili ya Mwafrika yatakayofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Sal...
-
Archeological and modern genetic evidence suggest that human populations have migrated into the Indian subcontine...
-
AGOSTI 31 mwaka huu kulikuwa na Maadhimisho ya Siku ya Tiba Asili ya Mwafrika yaliyofanyika Zanzibar katika viwanja vya Bustani ya Vi...
-
· Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa · Afisa Maendeleo wa Mtaa · Mwenyekiti wa Kamati ya Afya na Mazingira · ...