Tuesday, 21 October 2014
On 14:00 by Unknown No comments
WASHIRIKI katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa
ya Tiba Asili ya Mwafrika yatakayofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
Salaam Novemba 16 hadi 23 wametakiwa kuonyesha bidhaa bora ambazo zitaleta
ushindani katika soko la Tiba Asili.
Maonyesho hayo yanafanyika nchini kwa mara ya kwanza
na kuandaliwa na Jukwaa la Tiba Asili Tanzania kushirikiana, Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE).
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maonyesho
hayo, Boniventure Mwalongo alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa maonyesho
hayo yanatoa fursa kwa wadau mbalimbali wa Tiba Asili na Tiba Mbadala kuonyesha
bidhaa zenye viwango kama mwanzo wa kupeana changamoto lakini pia kudhihirisha ubora wa bidhaa za
Tiba Asili na Tiba Mbadala.
“Tunaka kuona bidhaa zenye ubora kuanzia katika
ufungashaji, maelekezo sahihi kuhusu matumizi lakini pia bidhaa hizo ziwe
zinafaa kwa matumizi ya binadamu ikiwa ni pamoja na kuwa na viwango
vinavyotakiwa,” alisema Mwalongo.
Mwalongo alichukua fursa hiyo kuwaomba Baraza la
Tiba Asili na Tiba Mbadala kutoa taarifa ya maonyesho hayo kwa waratibu wa
mikoa na wilaya ili nao waweze kuwataarifu watabibu wa Tiba Asili na Mbadala
waliosajiliwa katika maeneo yao ili waweze kushiriki kirahisi katika maonyesho
hayo.
“Njia hii itakuwa bora zaidi kwasababu
itawarahishishia washiriki kupata fomu kutoka kwa waratibu wao wa wilaya au
mkoa ambao pia wanawatambua kisheria,” alisema Mwalongo.
Washiriki katika maonyesho hayo ni pamoja na Watabibu
wa Tiba Asili, Watengenezaji wa Dawa Asili, Wakunga wa Tiba Asili, Kampuni za
Dawa Asili na vipodozi vya dawa asili, Wasambazaji wa Vifaa vya Tiba Asili na Tiba Mbadala,
Watengenezaji wa vyakula asili, kliniki za tiba asili na Tiba Mbadala.
Aidha kuna taratibu nyingine za kuyashirikisha
mashirika mengine ya kibiashara, taasisi binafsi za za serikali ili kutoa
nafasi ya kutangaza biashara zao kupitia maonyesho hayo ambayo yatashirikisha
wadau wa Tida Asili na Tiba Mbadala kutoka ndani na nje ya nchi.
Kwa mujibu wa Mwalongo, hadi sasa kuna baadhi ya
kampuni na taasisi ambazo zimeonyesha mwelekeo wa kutaka kudhamini maonyesho hayo
na kuwa taarifa rasmi itatolewa baada ya kufikia makubaliano.
Mbali na kutangaza Tiba Mbadala na Tiba Asili kwa
mapana yake, Mwalongo alisema kuwa wanataka kujenga mtandao mkubwa wa
kibiashara katika huduma ya Tiba Asili na Tiba Mbadala kwa nchi za Afrika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Mkurugenzi wa Kampuni ya Boresa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Tiba Asili Tanzania Tabibu Boniventura Mwalongo akitoa salam za pongezi kumpongeza Mhe. DKT John Pombe Joseph Magufuli kwa Kuchaguliwa Kuwa Raisi wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo tarehe 5 Novemba 2015 katika sherehe za kuapishwa kwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
kipanya
Popular Posts
-
TUJIKUMBUSHE YALE MAAJABU SABA YA DUNIA YA MWAKA 2007 Na Alberto sanga endelea...
-
habari zilizotufikia,Samaki huyu adimu kabisa duniani kumtia machoni ameonekana amefariki ama amekufa pembeni mwa ufukwe wa baha...
-
WAGANGA na wakunga wa tiba asili ni miongoni mwa watoa huduma za afya mbadala nchini ambapo wanaongozwa na sheria, mila, desturi na tarati...
-
WATAALAMU WA TIBA ASILI WAKUTANA CHINI YA JUKWAA MOJA; WAONYESHA UMAHIRI KATIKA TIBA ASILI NA MBADALA Mratibu wa Jukwaa la Tiba Asil...
-
FAHAMU KUHUSU TIBA A SILIA YA KUUNGANISHA MIFUPA Watu wengi wanao pata ajali za barabarani na kuvunjika viungo ...
-
WASHIRIKI katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Tiba Asili ya Mwafrika yatakayofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Sal...
-
Archeological and modern genetic evidence suggest that human populations have migrated into the Indian subcontine...
-
AGOSTI 31 mwaka huu kulikuwa na Maadhimisho ya Siku ya Tiba Asili ya Mwafrika yaliyofanyika Zanzibar katika viwanja vya Bustani ya Vi...
-
· Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa · Afisa Maendeleo wa Mtaa · Mwenyekiti wa Kamati ya Afya na Mazingira · ...
0 comments:
Post a Comment