Monday, 7 July 2014
On 01:21 by Unknown No comments
Mungu alipoamrisha watu tufunge alikuwa na maana kubwa, ingawa baadhi ya waumini wanafunga ili kutimiza nguzo ya dini na pengine wengine hufunga huku wakiona kama ni adhabu na wangependa mwezi umalizike haraka, lakini hata tafiti kadhaa za kisayansi zimegundua kwamba funga huimarisha afya kwa kutibu na kuzui baadhi ya magonjwa.
Kiasili, miongoni mwa tiba asilia zenye nguvu ya kupambana na kutibu maradhi mengi mwilini ni funga. Watu wengi hivi sasa wameshaanza kugundua siri ya funga ambayo huwa dawa ya haraka kwa magonjwa mepesi kama vile mafua, kichwa, wasiwasi, n.k ambayo kwa mfungaji huwa hayana nafasi.
Inaelezwa na wataalamu wa tiba asilia ya Yoga kuwa funga ndiyo njia rahisi ya kuondoa sumu mwilini iliyorundikana kwa muda mrefu kutokana na ulaji wa vyakula usio sahihi. Utashangaa wakati wa funga utakapogundua kuwa mwili unahitaji kiasi kidogo sana cha chakula kila siku, kwani utajikuta una afya njema na ulaji wako ni wa kiasi kidogo tofauti na siku zingine.
Dalili moja wapo ya mtu mwenye tatizo litokanalo na mwili kuwa na sumu nyingi mwilini kutokana na vyakula anavyokula, ni kukosa hamu ya kula (appetite). Katika hili hakuna dawa zaidi ya kukaa bila kula ili kupata hamu ya kula.
Kukosa hamu ya kula ni njia moja wapo inayotumiwa na mwili kutoa taarifa kwamba sehemu kadhaa za viungo vya mwili zimejaa sumu, hivyo mwili unalazimika kutumia njia zake za asili kuzuia kuendelea kuingia kwa sumu na badala yake kufanya jitihada za kuitoa sumu nje.
Kwa mantiki hiyo, funga inakubalika kabisa na ile ‘filosofia’ inayosababisha magonjwa. Ikiwa magonjwa yanasababishwa na kurundikana kwa sumu katika mfumo wa mwili, ambayo huingia kwa njia ya vyakula tunavyokula, inaingia akilini pia kutumia funga kuondoa mrundikano huo wa sumu mwilini.
JE, MAZOEZI YANARUHUSIWA WAKATI WA FUNGA?
Kuna dhana kwamba mtu anayefunga hatakiwi kujishughulisha, badala yake anatakiwa kupumzika. Dhana hii siyo kweli na ni kosa kubwa kuacha kujishughulisha au kufanya mazoezi wakati wa funga.
Hakuna sababu yoyote ya msingi mtu asijishughulishe na kazi zake za kila siku kama kawaida, muhimu ni kuzingatia uwezo wako wa kufanya shughuli au mazoezi hayo bila mwili kuishiwa nguvu kabisa.
AINA ZA FUNGA
Kuna aina kadhaa za funga ambazo mtu anaweza kuzitumia kwa lengo fulani. Funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni funga ya ibada, ambapo mfungaji anapata thawabu kwa Muumba wake lakini pia anapata faida za kiafya za ujumla zinazotokana na funga.
Aina hii ya funga inajulikana pia kama DRY FAST, kwa maana mtu hatakiwi kula wala kunywa kitu chochote kuanzia alfajiri hadi magharibi jua linapozama, kwa muda wa siku 30 au 29. Mfungaji wa funga aina hii, licha ya kuwa ni ibada, anapata pia faida zote za kiafya tulizozieleza hapo juu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Mkurugenzi wa Kampuni ya Boresa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Tiba Asili Tanzania Tabibu Boniventura Mwalongo akitoa salam za pongezi kumpongeza Mhe. DKT John Pombe Joseph Magufuli kwa Kuchaguliwa Kuwa Raisi wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo tarehe 5 Novemba 2015 katika sherehe za kuapishwa kwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
kipanya
Popular Posts
-
TUJIKUMBUSHE YALE MAAJABU SABA YA DUNIA YA MWAKA 2007 Na Alberto sanga endelea...
-
habari zilizotufikia,Samaki huyu adimu kabisa duniani kumtia machoni ameonekana amefariki ama amekufa pembeni mwa ufukwe wa baha...
-
WAGANGA na wakunga wa tiba asili ni miongoni mwa watoa huduma za afya mbadala nchini ambapo wanaongozwa na sheria, mila, desturi na tarati...
-
WATAALAMU WA TIBA ASILI WAKUTANA CHINI YA JUKWAA MOJA; WAONYESHA UMAHIRI KATIKA TIBA ASILI NA MBADALA Mratibu wa Jukwaa la Tiba Asil...
-
FAHAMU KUHUSU TIBA A SILIA YA KUUNGANISHA MIFUPA Watu wengi wanao pata ajali za barabarani na kuvunjika viungo ...
-
WASHIRIKI katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Tiba Asili ya Mwafrika yatakayofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Sal...
-
Archeological and modern genetic evidence suggest that human populations have migrated into the Indian subcontine...
-
AGOSTI 31 mwaka huu kulikuwa na Maadhimisho ya Siku ya Tiba Asili ya Mwafrika yaliyofanyika Zanzibar katika viwanja vya Bustani ya Vi...
-
· Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa · Afisa Maendeleo wa Mtaa · Mwenyekiti wa Kamati ya Afya na Mazingira · ...
0 comments:
Post a Comment