Friday, 25 July 2014

On 02:34 by Unknown   No comments
WAJASIRIAMALI zaidi ya 250 wanatarajia kushiriki kwenye maonyesho ya Nguvu Kazi/Jua Kali yatakayofanyika jijini Kigali, Rwanda kuanzia Novemba 30 hadi Desemba 7.
pix 3

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Msemaji wa Wizara ya Kazi na Ajira, Ridhiwan Wema, alisema fomu za maombi ya wajasiriamali kwenda kwenye maonyesho hayo zinapatikana kwenye ofisi zote za makatibu tawala wa mikoa (RAS).
Kwa mujibu wa Wema, lengo la maonyesho hayo ni kuongeza ajira, kuchochea ubunifu, kupanua wigo wa masoko kwa bidhaa za Tanzania nje ya nchi na kurasimisha shughuli za sekta isiyo rasmi.
pix 1
Alisema maonyesho hayo yalianza mwaka 1999 yakishirikisha nchi tano wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, na kwamba yanafanyika kwa mzunguko huku akibainisha kwamba mwaka jana yalifanyika jijini Nairobi, Kenya.
pix 2
“Tangu kuanza kwa maonyesho hayo, nguo kutoka Tanzania na bidhaa zinazotengenezwa kwa mikono zinafanya vizuri, ndiyo maana hata idadi ya washiriki inaongezeka kutoka 87 mwaka 1999 hadi wajasiriamali 113 mwaka jana,” alisema.
Katika maonyesho hayo, Wizara ya Kazi inashirikiana na wizara za Ustawi wa Jami, Vijana, Wanawake na Watoto ya Zanzibar, Afrika Mashariki, Uwezeshaji, Viwanda na Biashara, Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), TBS, TFDA na Mkurabita.
Alisema changamoto inayowakabili wajasiriamali wanaoshiriki maonyesho hayo ni rasilimali fedha zinazowafanya kushindwa kupanua wigo wa ubora na biashara zao.

0 comments:

Post a Comment

Mkurugenzi wa Kampuni ya Boresa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Tiba Asili Tanzania Tabibu Boniventura Mwalongo akitoa salam za pongezi kumpongeza Mhe. DKT John Pombe Joseph Magufuli kwa Kuchaguliwa Kuwa Raisi wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo tarehe 5 Novemba 2015 katika sherehe za kuapishwa kwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli

kipanya

Popular Posts