Monday, 11 August 2014

On 06:07 by Unknown   No comments

KWA UFUPI
Kingunge alisema ili utafiti ufanyike, ni lazima wawepo watu ambao wana taaluma hiyo na pia wapende fani hiyo na hali hicho ndicho kilichozifanya India, China na Vietnam kupiga hatua katika tiba za asilia.


Mlezi wa Chama cha Utabibu wa Tiba za Asili (ATME), Kingunge Ngombale Mwiru akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana. Picha na Joseph Zablon 
Dar es Salaam. Serikali imetakiwa kutoa fedha kwa ajili ya utafiti wa dawa asilia ili kusaidia jamii kukabiliana na maradhi.
Akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari uliofanyika Dar es Salaam jana, Mlezi wa Chama cha Utabibu wa Dawa za Asili Tanzania (ATME), Kingunge Ngombale Mwiru alisema utafiti ndiyo utakaowezesha kupiga hatua nzuri ya kupata tiba ya maradhi mbalimbali kwa kutumia tiba asilia.
Alisema Tanzania kuna dawa nyingi za tiba asilia ambazo zina matokeo mazuri na ya haraka pengine kuliko zile za kisasa, lakini hakuna utafiti unaofanyika na matokeo yake hakuna maendeleo yanayofikiwa na waganga hao wa tiba asili kubaki wakifanya kile ambacho kilikuwa kinafanywa na wazee wao.
“Kushindikana kwa utafiti kwa sababu ya ukosefu wa fedha kunafanya kukosekane maendeleo na badala yake tutakuwa tunarudia waliyogundua wazee wetu. Tukitaka kwenda mbele lazima kusimamia waliyoyagundua wao na kuendelea mbele,” alisema.
Kingunge alisema ili utafiti ufanyike, ni lazima wawepo watu ambao wana taaluma hiyo na pia wapende fani hiyo na hali hicho ndicho kilichozifanya India, China na Vietnam kupiga hatua katika tiba za asilia.
“Mathalan, pumu katika hospitali inasemwa kuwa hakuna tiba yake zaidi ya ile ya kutuliza, lakini mtaani unasikia kuna mtu anatibu pumu na pia kuna watu wengi katika maeneo tofauti ambao wanatibu magonjwa mbalimbali, lakini mwendelezo hakuna kwa kuwa hakuna mafungu ya utafiti.”
Alisema vijana wengi wasomi nchini wanafanya utafiti, lakini ni kwa maelekezo ya taasisi za nje kwa kuwa zina fedha.
Awali, Mwenyekiti wa ATME, Simba Abdulrahman Simba alisema kuna dawa nyingi za tiba za asili ambazo zina matokeo mazuri kuliko inavyofikiriwa na akaitaka Serikali kuruhusu dawa za jadi kutolewa hospitalini kama ilivyo nchi nyingine
.

0 comments:

Post a Comment

Mkurugenzi wa Kampuni ya Boresa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Tiba Asili Tanzania Tabibu Boniventura Mwalongo akitoa salam za pongezi kumpongeza Mhe. DKT John Pombe Joseph Magufuli kwa Kuchaguliwa Kuwa Raisi wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo tarehe 5 Novemba 2015 katika sherehe za kuapishwa kwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli

kipanya

Popular Posts