Wednesday, 13 August 2014
On 00:23 by Unknown No comments
MGANGA WA JADI ADAIWA KUMKATA MKONO ALIBINO HUYU AKIWA NA WENZAKE KISHA KUTOKOMEA KUSIKOJULIKANA NA MKONO HUO
Ukatili
dhidi ya wenye ulemavu wa ngozi (Albino) umejitokeza tena mkoani Tabora
ambapo mtoto Pendo Sengerema (14) mwanafunzi wa darasa la sita shule ya
msingi Nundu, amekatwa mkono wake wa kulia na wahalifu kukimbia nao
kusikojulikana na aliyeshiriki uharifu huo akihaidiwa kulipwa laki tisa
huko katika kijiji cha Usinge wilayani Kaliua.
Akiongea
kwa tabu alipolazwa katika hospitali ya wilaya ya Urambo mkoani Tabora
majeruhi Pendo Sengerema amesema kuwa, aliyemkata mkono alimfahamu maana
ni jirani anayesadikiwa kuwa, ni mganga wa kienyeji, ambapo kaimu
mganga wa hospitali hiyo, Dokta James Kang’oma, akidai kuwa walijitahidi
kuokoa maisha yake kutokanana kutoka kuvuja damu nyingi.
Mratibu
wa chama cha wenye ulemavu wa ngozi wilaya za Urambo na Kaliua Bw Focus
Mgesera, amesema kuwa, pamoja na mtoto huyo kulazwa katika hospitali
hiyo bado kuna hali ya hatali kwake kwani kwa namna moja ama nyingine
anaweza kuuawa kutokana na kuwafahamu waliomjeruhi, hivyo anahitaji
ulinzi.
Mkurugenzi
mtendaji wa shirika la Under the same sun, Bi Vicky Ntetemya aliyefika
hospitalini hapo kumwona mtoto huyo amesema kuwa, serikali iwe makini na
jamii ya wenye ulemavu wa ngozi kutokana na masuala ya wagombea nafasi
za uongozi kujishirikisha ma mambo ya waganga wa kienyeji.
Chama
cha walemavu wa ngozi nchini kimeraani tukio hilo kikitaka serikali
kuongeza ulinzi kwa jamii hiyo ambapo akizungumza kwa njia ya simu,
kamanda wa polisi mkoani Tabora Suzan Kaganda akidhibitisha kutokeaa
tukio hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Mkurugenzi wa Kampuni ya Boresa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Tiba Asili Tanzania Tabibu Boniventura Mwalongo akitoa salam za pongezi kumpongeza Mhe. DKT John Pombe Joseph Magufuli kwa Kuchaguliwa Kuwa Raisi wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo tarehe 5 Novemba 2015 katika sherehe za kuapishwa kwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
kipanya
Popular Posts
-
TUJIKUMBUSHE YALE MAAJABU SABA YA DUNIA YA MWAKA 2007 Na Alberto sanga endelea...
-
habari zilizotufikia,Samaki huyu adimu kabisa duniani kumtia machoni ameonekana amefariki ama amekufa pembeni mwa ufukwe wa baha...
-
WAGANGA na wakunga wa tiba asili ni miongoni mwa watoa huduma za afya mbadala nchini ambapo wanaongozwa na sheria, mila, desturi na tarati...
-
WATAALAMU WA TIBA ASILI WAKUTANA CHINI YA JUKWAA MOJA; WAONYESHA UMAHIRI KATIKA TIBA ASILI NA MBADALA Mratibu wa Jukwaa la Tiba Asil...
-
FAHAMU KUHUSU TIBA A SILIA YA KUUNGANISHA MIFUPA Watu wengi wanao pata ajali za barabarani na kuvunjika viungo ...
-
WASHIRIKI katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Tiba Asili ya Mwafrika yatakayofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Sal...
-
Archeological and modern genetic evidence suggest that human populations have migrated into the Indian subcontine...
-
AGOSTI 31 mwaka huu kulikuwa na Maadhimisho ya Siku ya Tiba Asili ya Mwafrika yaliyofanyika Zanzibar katika viwanja vya Bustani ya Vi...
-
· Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa · Afisa Maendeleo wa Mtaa · Mwenyekiti wa Kamati ya Afya na Mazingira · ...
0 comments:
Post a Comment