Sunday, 19 October 2014
On 01:39 by Unknown No comments
MAONYESHO YA TIBA ASILI KIMATAIFA KUFANYIKA DAR
NA MWANDISHI WETU, Dar
MAONYESHO ya Biashara ya Kimataifa ya Tiba Asili ya
Mwafrika yamepangwa kufanyika jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Mnazi
Mmoja kuanzia Novemba 16 hadi 23.
Maonyesho hayo ambayo yanafanyika nchini kwa mara
ya kwanza yameandaliwa na Jukwaa la Tiba Asili Tanzania kwa kushirikiana na
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Mamlaka ya ya Maendeleo ya Biashara
Tanzania (TANTRADE).
Mwenyekiti wa Kamati ya Manndalizi ya Maonyesho
hayo, Boniventure Mwalongo alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa wadau
mbalimbali wa Tiba Asili na Tiba Mbadala wanatarajia kushiriki katika maonyesho
hayo.
Kwa mujibu wa Mwalongo washiriki hao ni pamoja na
Watabibu wa Tiba Asili, Watengenezaji wa Dawa Asili, Wakunga wa Tiba Asili,
Kampuni za Dawa Asili na vipodozi vya dawa asili, Wasambazaji wa Tiba Asili na
Tiba Mbadala, Watengenezaji wa vyakula asili, kliniki za tiba asili na Tiba
Mbadala.
Aidha mwalongo alisema kuwa wanaendelea na taratibu
za kufanya maongezi na wadhamini mbalimbalia ambapo watatoa taarifa rasmi baada
ya kufikia tamati ya maongezi, ikiwa ni pamoja na kutoa ratiba nzima ya
maonyesho hayo.
“Tunafanya maongezi na wadau mbalimbali ambao
wameonyesha nia ya kutusaidia, lakini pia kauli mbiu ya mwaka huu ni
‘Ushirikiano wa Tiba Asili na Tiba za kisasa katika kuhimarisha huduma ya Afya
Afrika’, alisema Mwalongo.
Aliongezea kuwa hadi sasa wana orodha wadau
wasiopungua 280 ambao tayari wameonyesha nia ya kushiriki katika maonyesho
hayo, baada ya kuwapelekea taarifa kwa njia mbalimbali za mawasiliano.
Kwa mujibu wa Mwalongo, gharama za kushiriki zimegawantika
katika makundi tofauti ambapo Watambuzi wa magonjwa, watengenezaji wa dawa
asili, wakunga wa tiba asili, Wenye virutubisho vya tiba asili na wauzaji
wa dawa asili gharama yao ni
100,000/-. Kampuni za dawa asili na vipodozi asili zitalipa 500,000/-.
Wasambazaji wa dawa za asili na dawa mbadala
watatakiwa kulipa ada ya 1,000,000/-. Wauza vyakula asili watalipia
150,000/- wakati kliniki ya tiba asili watalipia 1,500,000/- Kliniki ya tiba
mbadala gharama yake ni
2,000,000/-. Kampuni za virutubisho kutoka nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
zitalipia dola za Marekani 1,500.
Viwango vingine ni dola 500 za Marekani kwa Kampuni
za Tiba Asili ndani ya Jumuiya ya Afrika Mshariki. Gharama za ushiriki kwa Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
na Taasisi za Serikali ni 2,000,000/-. Wajasiliamali wa kazi za uchongaji
watalipia 500,000, wakati vyama vya tiba asili vitalipia 1,000,000.
Aidha Mwalongo alitoa wito kwa makundi mengine
ambayo yangependa kushiriki, kujitokeza mapema ili taratibu ziweze kufuatwa.
“Huenda kuna makundi mengine ambayo labda tumeyasahau, lakini milango bado iko
wazi kwa yeyote ambaye angependa kushiriki maonyesho haya,” alisisitiza
Mwalongo.
Alisema kuwa wana imani baada ya maonyesho hayo
kutakuwa na mtandao mkubwa wa kibiashara katika huduma ya tiba asili na tiba
mbadala kwa nchi za Afrika na hata nje ya Afrika. Aidha alisema kuwa wako
mbioni kuyasajili rasmi maonyesho hayo ili yawe yanafanyika kila Agosti 30 pale
inapoadhimishwa siku tiba Asili ya Mwafrika.
Ends.
GHARAMA ZA VIWANGO VYA USHIRIKI WA MAONYESHO YA KWANZA
YA KIMATAIFA YA TIBA ASILI YA MWAFRIKA TAREHE 16- 23
NOVEMBA 2014
Na.
|
Washiriki wa ndani
|
Gharama
T.shs.
|
Washiriki wa nje ya nchi
|
USD
|
1.
|
Watambuzi wa Magonjwa
|
100,000/=
|
EAC
|
500
|
Watengenezaji wa Dawa
|
100,000/=
|
Nje ya EAC
|
1,500
|
|
Wakunga wa Asili
|
100,000/=
|
|||
Wenye Virutubisho vya Asili
|
100,000/=
|
|||
Wauzaji wa Dawa Asili
|
100,000/=
|
|||
Wajasiriamali
|
100,000/=
|
|||
Vyakula vya Asili
|
150,000/=
|
|||
Makampuni ya Dawa Asili na
Vipodozi
|
500,000/=
|
|||
Wasanii (Wachongaji wa
Vinyago)
|
500,000/=
|
|||
Wasambazaji wa Vifaa vya
Tiba Asili na Tiba Mbadala na (Dawa za Kisunna)
|
1,000,000/=
|
|||
Vyama vya Tiba Asili
|
1,000,000/=
|
|||
Kliniki ya Tiba Asili
|
1,500,000/=
|
|||
Makampuni ya virutubisho
|
1,500,000/=
|
|||
Kliniki ya Tiba Mbadala,
Benki,
Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
na Taasisi za Serikali, Makampuni ya Vifungashio.
|
2,000,000/=
|
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Mkurugenzi wa Kampuni ya Boresa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Tiba Asili Tanzania Tabibu Boniventura Mwalongo akitoa salam za pongezi kumpongeza Mhe. DKT John Pombe Joseph Magufuli kwa Kuchaguliwa Kuwa Raisi wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo tarehe 5 Novemba 2015 katika sherehe za kuapishwa kwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
kipanya
Popular Posts
-
TUJIKUMBUSHE YALE MAAJABU SABA YA DUNIA YA MWAKA 2007 Na Alberto sanga endelea...
-
habari zilizotufikia,Samaki huyu adimu kabisa duniani kumtia machoni ameonekana amefariki ama amekufa pembeni mwa ufukwe wa baha...
-
WAGANGA na wakunga wa tiba asili ni miongoni mwa watoa huduma za afya mbadala nchini ambapo wanaongozwa na sheria, mila, desturi na tarati...
-
WATAALAMU WA TIBA ASILI WAKUTANA CHINI YA JUKWAA MOJA; WAONYESHA UMAHIRI KATIKA TIBA ASILI NA MBADALA Mratibu wa Jukwaa la Tiba Asil...
-
FAHAMU KUHUSU TIBA A SILIA YA KUUNGANISHA MIFUPA Watu wengi wanao pata ajali za barabarani na kuvunjika viungo ...
-
WASHIRIKI katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Tiba Asili ya Mwafrika yatakayofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Sal...
-
Archeological and modern genetic evidence suggest that human populations have migrated into the Indian subcontine...
-
AGOSTI 31 mwaka huu kulikuwa na Maadhimisho ya Siku ya Tiba Asili ya Mwafrika yaliyofanyika Zanzibar katika viwanja vya Bustani ya Vi...
-
· Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa · Afisa Maendeleo wa Mtaa · Mwenyekiti wa Kamati ya Afya na Mazingira · ...
0 comments:
Post a Comment