Sunday, 29 June 2014

On 23:25 by Unknown   No comments


Mratibu wa Chama cha Watabibu wa Dawa Asili Tanzania (ATME) Mkoa wa Mbeya,Boniventura Mwalongo, alisema baadhi ya watu hutumia majina wa waganga kufanya uhalifu tofauti na matakwa ya watanzania.
Zahra Mansour akisoma tamko la  kulaani vitendo vya kinyama na kikatili vinavyokiuka sheria za nchi vinavyofanywa na waganga wa kienyeji kama ilivyotokea Mkoani Mwanza Oktoba 28 Mwaka huu kwa Waganga wawili wa Kienyeji na mkulima mmoja kukamatwa wakiwa na kuingo cha binadamu wakitaka kukiuza kwa shilingi milioni moja.
Mzee  A. Mgaya



WATANZANIA wametakiwa kuwa makini na kutofautisha shughuli za waganga wa jadi, waganga wa tiba asili na waganga wa kienyeji zinazopotosha jamii.
Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni Mratibu wa Chama cha Watabibu wa Dawa Asili Tanzania (ATME) Mkoa wa Mbeya,Boniventura Mwalongo, alisema baadhi ya watu hutumia majina wa waganga kufanya uhalifu tofauti na matakwa ya watanzania.
Alisema baadhi ya matendo kama biashara haramu ya viungo vya binadamu na mauaji ya Albino, Vikongwe, upigaji nondo, utoaji utajirisho, fedha za majini, kuunganisha watu na freemason, rambaramba, kuzuza na kuruka na ungo siyo sehemu ya shughuli za tiba asili.
Alisema tiba asili inatambuliwa kwa mujibu wa sheria namba 23 ya mwaka 2002, hivyo waganga wa kienyeji wanatumia utapeli kuwarubuni wananchi kwa kuigiza kama matabibu wa tiba asili.
Alisema Watabibu wa tiba asili Mkoa wa Mbeya wanatoa wito kwa taasisi zinazojihusisha na tiba asili kutojitambulisha kama waganga wa tiba asili na badala yake wajitambulishe kama watabibu wa tiba asili.
Alisema utambulisho wa mganga wa tiba asili unatumika vibaya na baadhi ya madui wa tiba asili na kupelekea wananchi kuelewa na kuwatambua kama Waganga wa jadi, waganga wa tiba asili na waganga wa kienyeji kama wamoja ambapo wanatofautiana kwa matendo na ueledi wao pamoja na sifa na ujuzi wao.
Mratibu huyo aliongeza kuwa ni wakati wa Watatibu wa Tiba asili kote nchini kusajiliwa kwa mujibu wa sheria ili kuwakomesha na kukemea kwa nguvu wanaowahujumu kwa kujihusisha na vitendo vya ushirikina na mambo yanayoipotosha jamii.
Alisema kila mtabibu anapaswa kuwa mlinzi wa maadili ya taaluma yake kwa mujibu wa sera, sheria kanuni na miongozo iliyopo.
Aidha alitoa wito kwa Vyombo vya Dola kuwafungulia milango ya ushirikiano ili kukabiliana na vitendo vya kidhalimu vinavyoihusisha tiba asili  ili kuzuia athari zinazoweza kujitokeza kutokana na matumizi mabaya ya taaluma ya tiba asili.
Katika mkutano huo ambao ulikuwa unalengo la kulaani vitendo vya kinyama na kikatili vinavyokiuka sheria za nchi vinavyofanywa na waganga wa kienyeji kama ilivyotokea Mkoani Mwanza Oktoba 28 Mwaka huu kwa Waganga wawili wa Kienyeji na mkulima mmoja kukamatwa wakiwa na kuingo cha binadamu wakitaka kukiuza kwa shilingi milioni moja.

0 comments:

Post a Comment

Mkurugenzi wa Kampuni ya Boresa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Tiba Asili Tanzania Tabibu Boniventura Mwalongo akitoa salam za pongezi kumpongeza Mhe. DKT John Pombe Joseph Magufuli kwa Kuchaguliwa Kuwa Raisi wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo tarehe 5 Novemba 2015 katika sherehe za kuapishwa kwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli

kipanya

Popular Posts