Tuesday, 8 July 2014

On 01:17 by Unknown   No comments

Mwenyekiti wa Chama Cha Watabibu wa Tiba Asilia Tanzania, Simba Abdulrahaman Simba (wa pili kushoto) akiongea na wanahabari (hawapo pichani) katika ukumbi uliopo kwenye Hoteli ya Travetine, Magomeni jijini Dar.
Wajumbe walikuwa meza kuu wakisikiliza maswali kutoka kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).
---
22 AGOSTI 2013
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MAADHIMISHO YA SIKU YA TIBA ASILI YA MWAFRIKA
KAULI MBIU: “TIBA ASILI, UTAFITI NA MAENDELEO”
1.     Maadhimisho ya siku ya tiba ya Mwafrika huadhimishwa kila mwaka tarehe 31 Agosti 2013. Inaadhimishwa na nchi 46 za Bara la Afrika. Siku ya Tiba Asili ya  Mwafrika tarehe 31 Agosti  ya  kila  mwaka Serikali na Wananchi watambue kuwa ni JUKWAA la Tiba Asili na kutathmini maendeleo ya Tiba Asili nchini.

2.    Maadhimisho ya siku ya Tiba Asili ya Mwafrika yaliadhimishwa kwa  mara ya kwanza tarehe 31 Agosti 2003 hapa nchini. Mwaka huu ni maadhimisho ya 10, Nachukua  fulsa hii  kuwaalika katika kupata fedha za maadhimisho ya Tiba Asili ya Mwafrika ya mwaka huu 2013. Kama  tulivyokubaliana katika  Mkutano wa pamoja ulifanyika katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii tarehe 14/08/2013 kuwa wadau wa Tiba za  Asili tushiriki katika kuwezesha kupata fedha za kuwezesha maadhimisho ya mwaka huu kufanyika. Maadhimisho ya mwaka huu kauli mbiu: ‘Tiba Asili , Utafiti na Maendeleo’ ambayo yatafanyika katika Uwanja  wa Mnazi Mmoja.
Watanzania kupitia maadhimisho hayo wataweza kujua kuhusu Tiba Asili inatambuliwa kwa mujibu wa sheria na. 23 ya mwaka 2002 na kanuni na miongozo  yake .

3.    Maadhimisho ya siku ya Tiba ya Asili  ya Mwafrika yamekuwa yakidhaminiwa na Serikali, Mwaka  huu Serikali imeshirikisha Waganga  na Wakunga  wa Tiba Asili katika kugharamia gharama za kufanikisha ufanisi wa siku ya Tiba Asili ya Mwafrika . Kwa kupitia Vyama  vya Waganga na Wakunga na  Tiba Asili.

4.    ATME inaomba wanachama wote wa ATME  nchi nzima, Wadau wote, Makampuni yote  na Watu binafsi  wachangie ufanisi wa Maadhimisho ya Siku ya Tiba Asili ya Mwafrika kwa hali na mali ili Kuilinda , Kuitetea, Kuiboresha na Kuendeleza Tiba Asili nchini ili kupunguza ukiukwaji wa haki za binadamu.

5.    Mgeni Rasimi wa Maadhimisho ya Siku ya Tiba Asili ya Mwafrika tarehe 31Agosti 2013 ni Waziri  Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. MIZENGO KAYANZA PETER PINDA. (MB)

6.    Madhumuini ya Maadhimisho ya  Siku ya  Tiba Asili ya Mwafrika ni kuwaunganisha Waganga na Wakunga wa Tiba Asili nchini katika kufanya Utafiti wa dawa za Tiba Asili , Kuilinda , Kuitetea , Kuiboresha katika vigezo vya ubora , usalama na viwango ili kuendeleza Tiba Asili.

Pili kuelimisha Umma tofauti iliyopo kati ya Tiba Asili na Uchawi , Ramli chonganishi, uzushi na  aina yoyote ile inayokiuka haki ya binadamu na kuhusishwa na Tiba Asili.

Tatu maadhimisho ya  siku ya  Tiba Asili ya tarehe 31Agosti 2013  siku  ya  kuundwa  jukwaa la Tiba Asili  la kufanya Tathmini ya  Utafiti, Maboresho na Maendeleo ya Tiba Asili na Changamoto zake  nchini ni JUKWAA LA KITAIFA LA WADAU WA TIBA ASILI.

7.    Maonyesho ya siku ya Tiba Asili ya Mwafrika yataanza tarehe 15 Agosti 2013 hadi  tarehe 20 Agosti 2013 katika viwanja vya Mnazi  mmoja yatahusisha Waganga wa Tiba Asili na Wadau wa Tiba Asili.

8.    Katika Maadhimisho ya Siku ya  Tiba Asili ya Mwafrika , Mgeni rasmi Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda atatembelea Chuo Kikuu kishiriki cha Sayansiza Tiba Muhimbili (MUHAS) na Taasisi ya Utafiti  wa Dawa Asili Muhimbili (ITM), Duka la Dawa Asili Magomeni Kliniki ya Dawa Asili Kariakoo Mtaa wa Nyamwezi, Maduka ya Vifaa Tiba (Gala) Kariakoo, Kilinge cha Tiba Asili Wilaya ya Temeke.

9.    Watabibu na  Wakunga wa Tiba Asili tunafahamika ni miongoni mwa watoa huduma za Afya kwa kufuata sera, sheria , mila, desturi na taratibu za kiasili nchini. Sasa Tiba Asili inazungumzika na inatengana na imani zinazohatarisha usalama wa watu na mali zao kwa kuwa si  sehemu ya uchawi, ushirikina, mazingaombwe, upigaji ramli,  kuzuza kutoa uchawi kutoa utajirisho, kutengeneza fedha za majini ukeketaji kwa wanawake (tohara) , kufuta kesi zilizopo mahakamani, kuwarudishia watu vitu  vilivyopotea , kuwafufua wafu, kutoa mazindiko kwa  waharifu , kufuta  faili za kesi mbali mbali, kuruka na ungo kutoka eneo moja kwenda eneo jingine , uchunaji wa ngozi, upigaji nondo, mauaji ya albino, vikongwe  na  matumizi mabaya ya Taaluma ya Tiba Asili.
“Mmoja mmoja na  sote kwa pamoja tushirikiane kuiletea maendeleo nchi yetu”

Asante  “ Kwa kutusikiliza”
SIMBA ABDULRAHAMAN SIMBA
MWENYEKITI
CHAMA CHA WATABIBU WA TIBA ASILIA TANZANIA

0 comments:

Post a Comment

Mkurugenzi wa Kampuni ya Boresa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Tiba Asili Tanzania Tabibu Boniventura Mwalongo akitoa salam za pongezi kumpongeza Mhe. DKT John Pombe Joseph Magufuli kwa Kuchaguliwa Kuwa Raisi wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo tarehe 5 Novemba 2015 katika sherehe za kuapishwa kwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli

kipanya

Popular Posts