Tuesday, 8 July 2014

On 01:13 by Unknown   No comments



UONGOZI wa Umoja wa Waganga na Watabibu wa Tiba asili nchini umewataka watabibu wa tiba asili kujiunga na vyama vya waganga ili kufahamika kama watoa huduma katika maeneo wanayoishi.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Umoja huo Bw.Simba Abrahman wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye kikao cha makabidhiano ya fomu za usajili wa watabibu hao.

Bw.Abrahman amesema kuwa mpaka sasa watabibu 33 wameshajiandikisha kuchukua fomu za usajili kama agizo la Waziri Mkuu linavyosema sambamba na sheria ya Tiba Asili inavyotaka.

Aidha amewataka watabibu kutokubali kurubuniwa na kupewa vyeti feki bila kufata hatua zinazotakiwa ikiwa ni pamoja na kupeleka fomu kuthibitishwa na mjumbe wa mahali anapoishi.

“natoa wito kwa watu wasije kudanganyika na kupewa vyeti feki bila kufuata hatua zinazotakiwa ,tutashirikiana na wenzetu kuhakikisha waganga wote wanaotoa huduma wamesajiliwa na wanavibali.”Alisema Abrahaman

Ameongeza kuwa watabibu wenye mabango barabarani yanayoeleza magonjwa wanayotibu hawanabudi kuyatoa na kuweka mabango mapya kwani yanakiuka sheria ya Tiba asili ambayo inataka mtoa huduma hiyo kutaja jina lake , mahali anapopatikana na namba ya simu.

0 comments:

Post a Comment

Mkurugenzi wa Kampuni ya Boresa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Tiba Asili Tanzania Tabibu Boniventura Mwalongo akitoa salam za pongezi kumpongeza Mhe. DKT John Pombe Joseph Magufuli kwa Kuchaguliwa Kuwa Raisi wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo tarehe 5 Novemba 2015 katika sherehe za kuapishwa kwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli

kipanya

Popular Posts