Wednesday, 13 August 2014
On 00:31 by Unknown No comments
Mwanamke
mmoja nchini India ameogelea kwenye mto uliokuwa umejaa maji mengi
yaliyotokana na mvua kubwa ilhali akiwa na ujauzito wa miezi tisa.
Anasema sababu ya safari yake majini ni ili aweze kufika katika kituo cha afya aweze kujifungulia hospitalini.
Mama
huyo kwa jina Yellawa alitumia maboga makavu yenye maganda magumu
yaliyomsaidia kuogelea kwa umbali wa karibu kilomita moja kutoka kwenye
kijiji chake kusini mwa jimbo la Karnataka.
Alishikwa na uoga lakini alitaka kujifungua salama, hakuna kituo cha afya kijijini kwake na hakutaka kujifungulia nyumbani.
Wanakijiji na madaktari wamesifu hatua yake ya kuogelea kuwa ni mafanikio makubwa.
Yellawa
ni binti wa miaka 22, kutoka kijiji cha Neelakantarayanagadde, kijiji
kidogo kando kando ya mto Krishba kaskazini mwa mji wa Bangalore.
Namna
pekee ya kusafiri kutoka katika kijiji hicho kwa kuvuka mto ni kwa
kutumia miti iliyotengenezwa kwa kuunganishwa mithili ya boti, kifaa
ambacho hata hivyo si imara na hakifanyi kazi nyakati ambazo mto huwa
umejaa maji.
Wakati
Yellawa akiogelea kuvuka mto juma lililopita, maji yalikua yameongezeka
ambapo alishuhudia waogeleaji wakisita kuingia kwenye maji.
Binti huyu alishikwa na hofu lakini alijipa moyo kuwa anafanya vile kwa usalama wa mtoto wake.
Yellawa alisaidiwa na baba yake, kaka na ndugu zake ambao waliogelea pamoja naye.
Ingawa
alikua amechoka lakini daktari aliyekuwa akimchunguza alipowasili
katika hospitali ya serikali karibu na kijiji cha Kekkera alisema kuwa
anaendelea vizuri na yuko nyumbani kwa nduguye amepumzika.
Yellawa anasifiwa kwa ushujaa wake wa kuvuka mto kwa hali ya ujauzito aliokuwa nao
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Mkurugenzi wa Kampuni ya Boresa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Tiba Asili Tanzania Tabibu Boniventura Mwalongo akitoa salam za pongezi kumpongeza Mhe. DKT John Pombe Joseph Magufuli kwa Kuchaguliwa Kuwa Raisi wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo tarehe 5 Novemba 2015 katika sherehe za kuapishwa kwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
kipanya
Popular Posts
-
TUJIKUMBUSHE YALE MAAJABU SABA YA DUNIA YA MWAKA 2007 Na Alberto sanga endelea...
-
habari zilizotufikia,Samaki huyu adimu kabisa duniani kumtia machoni ameonekana amefariki ama amekufa pembeni mwa ufukwe wa baha...
-
WAGANGA na wakunga wa tiba asili ni miongoni mwa watoa huduma za afya mbadala nchini ambapo wanaongozwa na sheria, mila, desturi na tarati...
-
WATAALAMU WA TIBA ASILI WAKUTANA CHINI YA JUKWAA MOJA; WAONYESHA UMAHIRI KATIKA TIBA ASILI NA MBADALA Mratibu wa Jukwaa la Tiba Asil...
-
FAHAMU KUHUSU TIBA A SILIA YA KUUNGANISHA MIFUPA Watu wengi wanao pata ajali za barabarani na kuvunjika viungo ...
-
WASHIRIKI katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Tiba Asili ya Mwafrika yatakayofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Sal...
-
Archeological and modern genetic evidence suggest that human populations have migrated into the Indian subcontine...
-
AGOSTI 31 mwaka huu kulikuwa na Maadhimisho ya Siku ya Tiba Asili ya Mwafrika yaliyofanyika Zanzibar katika viwanja vya Bustani ya Vi...
-
· Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa · Afisa Maendeleo wa Mtaa · Mwenyekiti wa Kamati ya Afya na Mazingira · ...
0 comments:
Post a Comment