Wednesday, 13 August 2014
On 00:34 by Unknown No comments
Bw. Hamis Juma akijitetea kuhusiana na shutuma za mkewe.
“Na tangu mume
wangu aanze mchezo huo huyo mbwa mmoja mweusi (pichani) amenawiri kupita kiasi, naamini amempa mimba.
“Na tangu mume
Kweli
dunia sasa ni vululuvululu! Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina
la Cecilia Hamis (pichani), mkazi wa Majoe Mjimpya Relini jijini Dar es
Salaam amemlalamikia mumewe aliyemtaja kwa jina la Hamis Juma kwamba
ametembea na mbwa wao mweusi hadi kumpa mimba.Akizungumza na Uwazi mwishoni mwa wiki iliyopita nyumbani kwake, mwanamke huyo alisema alibaini hilo wiki mbili zilizopita.
SIMULIZI YENYEWE
“Nililigundua
hilo wiki mbili zilizopita. Nakumbuka ilikuwa usiku nikiwa nimelala,
nikamsikia mbwa mmoja (kati ya wawili) analia. Niliamka kwenda kuangalia
ili kujua sababu, kufika nikawasha tochi ya simu, nilishangaa sana
kumwona mume wangu yuko naye amemshikilia (asomaye na afahamu).
“Nilimuuliza anachokifanya, akasema anammalizia shida zake kwa kuwa hakuna mbwa wa kiume wa kumsaidia,” alisema mwanamke huyo.
MARA YA PILI
Akiendelea kumlalamikia mume wake kwa madai hayo mazito, mama huyo alisema:
“Siku
iliyofuata usiku tena, nikiwa nimelala nilimsikia mbwa akilia, nikaamka.
Safari hii niliambatana na watoto wangu, tukaenda nje, kufika
tukamshuhudia mume wangu akifanya tukio kama la jana yake, nilipomuuliza
akanipa majibu yaleyale kwamba anammaliza shida zake mbwa huyo.”
Akaendelea:
“Hawa mbwa waliletwa wawili wakiwa wadogo kabisa na wote ni majike na
tangu walipoletwa sijawahi kumwona mbwa dume hata siku moja kwani mara
nyingi tunawafungia kwenye banda lao.
”
AWAELEZA MAJIRANI
Mwanamke huyo
alisema kutokana na kukithiri kwa tabia hiyo, aliamua kuwaeleza
majirani ambao nao walimshauri aende kuripoti kwa mjumbe wa eneo hilo.
MJUMBE MWENYEWE HUYU HAPA
Akizungumza
na Uwazi, Mjumbe wa Shina Na. 26, Majoe Mjimpya, Mbaruka Nyamaishwa
alikiri kupokea malalamiko hayo kutoka kwa mwanamke huyo akamshauri
kuyapeleka kwenye Kituo cha Polisi cha Stakishari.
MAJIRANI WAONA ANACHELEWA
Habari zaidi
zinawekwa wazi kwamba, majirani nao walipoona mwanamke huyo anachelewa
kwenda polisi, wao walimsomba na kwenda naye ambapo walitoa taarifa
katika Dawati la Jinsia.
Mkuu wa
dawati hilo, Koplo Golbert aliongozana na walalamikaji hao hadi nyumbani
kwa mdaiwa ambapo alimkagua mbwa huyo na kuwaamuru wanandoa hao
kuripoti kwenye kituo hicho cha polisi bila kukosa jana Jumatatu saa 3
kuonana na mkuu huyo na uchunguzi kuendelea.
SWALI LA MSINGI
Uwazi
lilimuuliza swali moja mwanamke huyo, ni kwa nini anasema aliamka na
kutoka nje usiku bila kueleza mumewe anakuwa wapi muda huo kwani
hakuonyesha kushangaa kutomwona kitandani?
Anajibu: “Tulitengana vyumba kwa sababu ya ugomvi wa kifamilia.”
JE, MUME ANASEMAJE?
Uwazi lilimgeukia mume wa mwanamke huyo na kumuuliza kuhusu madai mazito ya mkewe ambapo alisema:
“Mimi
sijawahi kufanya kitendo hicho na mbwa ila nahisi mke wangu na hawa
majirani wa hapa wananitengenezea hilo tukio ili nikafungwe jela maisha,
halafu wao waweze kuchukuwa mashamba yangu kwani ndani ya ndoa yangu
kumekuwa na ugomvi wa mara kwa mara.”
UWAZI LAMUULIZA DAKTARI WA MUHIMBILI
Uwazi
lilitilia shaka uwezekano wa mbwa kunasa mimba ya binadamu, hivyo
lilimsaka daktari mmoja wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na
kumuuliza kuhusu madai ya mwanamke huyo.
Msikie: “Mh! Binadamu kumpa mimba mbwa haiwezekani. Binadamu anaweza kumpa mimba sokwe, kwa mbali sana nyani. Lakini si mbwa.
“Ila
kama huyo mama anasema hivyo, mbwa akapimwe na ikibainika ni kweli basi
yatakuwa maajabu ya dunia maana dunia ina mambo yake.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Mkurugenzi wa Kampuni ya Boresa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Tiba Asili Tanzania Tabibu Boniventura Mwalongo akitoa salam za pongezi kumpongeza Mhe. DKT John Pombe Joseph Magufuli kwa Kuchaguliwa Kuwa Raisi wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo tarehe 5 Novemba 2015 katika sherehe za kuapishwa kwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
kipanya
Popular Posts
-
TUJIKUMBUSHE YALE MAAJABU SABA YA DUNIA YA MWAKA 2007 Na Alberto sanga endelea...
-
habari zilizotufikia,Samaki huyu adimu kabisa duniani kumtia machoni ameonekana amefariki ama amekufa pembeni mwa ufukwe wa baha...
-
WAGANGA na wakunga wa tiba asili ni miongoni mwa watoa huduma za afya mbadala nchini ambapo wanaongozwa na sheria, mila, desturi na tarati...
-
WATAALAMU WA TIBA ASILI WAKUTANA CHINI YA JUKWAA MOJA; WAONYESHA UMAHIRI KATIKA TIBA ASILI NA MBADALA Mratibu wa Jukwaa la Tiba Asil...
-
FAHAMU KUHUSU TIBA A SILIA YA KUUNGANISHA MIFUPA Watu wengi wanao pata ajali za barabarani na kuvunjika viungo ...
-
WASHIRIKI katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Tiba Asili ya Mwafrika yatakayofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Sal...
-
Archeological and modern genetic evidence suggest that human populations have migrated into the Indian subcontine...
-
AGOSTI 31 mwaka huu kulikuwa na Maadhimisho ya Siku ya Tiba Asili ya Mwafrika yaliyofanyika Zanzibar katika viwanja vya Bustani ya Vi...
-
· Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa · Afisa Maendeleo wa Mtaa · Mwenyekiti wa Kamati ya Afya na Mazingira · ...
0 comments:
Post a Comment