Monday, 7 July 2014

On 23:33 by Unknown   1 comment
Serikali imepiga marufuku na kutaka kuondolewa mara moja mabango yote ya wataalam wa tiba asili yanayojitangaza kutibu maradhi ambayo hayajathibitishwa kitaalamu yaliyobandikwa maeneo mbalimbali nchini huku baadhi ya wabunge wakitishia kukwamisha bajeti ya wizara ya fedha endapo wizara hiyo haitatoa kiasi cha fedha cha zaidi ya asilimia 50 ya bajeti ya wizara ya afya na ustawi wa jamii.
Wakichangia mjadala wa bajeti ya wizara ya maji mara baada ya waziri mwenye dhamana pamoja na kamati ya bunge na kambi ya upinzani bungeni kuwasilisha maoni yao siku ya Jumamosi iliyopita baadhi ya wabunge wamesema licha ya kuwa Tanzania ina maeneo ambayo yanajulikana kuwa na matatizo makubwa ya maji kutokana na ukame bado mawaziri hao wamejitengea kiasi kikubwa cha fedha kutekeleza miradi ya maji licha ya kuwa maeneo hayo yanaunafuu ya upatikanaji wa maji pamoja na idadi ndogo ya watu.
Pia baadhi yao wamezitupia lawama mamlaka za miji za maji kwa kushindwa kutoa huduma ya maji kwa wananchi huku wafanyabiashara wa maji wanaotumia malori wakipata maji na kuwauzia wananchi kwa bei kubwa huku baadhi yao wakidhamiria kutoa hoja binafsi bungeni kujadili kauli ya waziri aliyoitoa bungeni kuwa tatizo la maji jijini Dar es salaam limepungua.
Mara baada ya bajeti ya wizara ya maji kupitishwa na bunge wizara ya afya na ustawi wa jamii hii leo nayo imewasilisha hotuba ya bajeti yake bungeni mjini Dodoma.

1 comment:

  1. Utajiri wa nguvu za ujihni na ndagu JE UNAMATATIZO, (KWANINI USUMBUKE) NAITWA DR, MDIRO piga 0742162843. KAMA UNAITAJI PESA ZA MAJINI AU NDAGU YA MALI AU UTAJIRI NDANI YA MASAA 72(SIKU TATU), NDOA, MIKOSI, MABALAA, JINI MAHABA NA SHIDA YA UZAZI. NIPIGIE 0742162843. KIKUBWA NI KUSIKILIZA NA KUFATA MASHARTI. ANGALIZO USITUME SMS PIGA NA UWE NA NIA.

    (kuhusu utajiri au pesa) KABLA YA KUPIGA SIMU ZINGATIA YAFUATAYO
    1. uwe una umri wa miaka 18+
    2. uwe tayari kupokea masharti yote
    3.uwe na uwezo wa kutunza siri
    4. uwe jasiri wa kupokea taarifa yoyote 

    ReplyDelete

Mkurugenzi wa Kampuni ya Boresa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Tiba Asili Tanzania Tabibu Boniventura Mwalongo akitoa salam za pongezi kumpongeza Mhe. DKT John Pombe Joseph Magufuli kwa Kuchaguliwa Kuwa Raisi wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo tarehe 5 Novemba 2015 katika sherehe za kuapishwa kwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli

kipanya

Popular Posts